Mwanamke ajaribu kugonga polisi akitumia gari Washington
Polisi mjini Washington nchini Marekani, wamemfyatulia risasi mwanamke mmoja aliyekuwa ndani ya gari, baada ya yeye kugonga gari la polisi karibu na bunge la Marekani na baadaye kujaribu kuwagonga maafisa kadha wa polisi.
Mwanamke huyo hakupigwa risasi, kwa mujihu wa msemaji wa polisi mjini Washington.
Alikamatwa na kisa hicho kikasababisha kufungwa kwa moja ya majengo ya bunge.
Kisa hicho kinajiri baada ya kushuhudiwa mashambulizi kadha ya kugonga kwa magari miji ya London na Brussels,
Msemaji wa polisi Eva Malecki, amesema kuwa mshukiwa ni mwanamke na kisa hicho ni cha uhalifu.Polisi wakiweka ulinzi katika bunge la Marekani
Kisa hicho kilitokea wakati maafisa waligundua dereva ambaye alikuwa akiendesha gari kwa njia isiyo ya kawaida na kutaka kumsimamisha.
Dereva huyo kisha akageuza gari kwa haraka na nusura awagonge polisi.
Sababaua ya kisa hicho haijulikani na mwanamke huyo hajatambuliwa.
Vikao vya bunge vinaendelea kama kawaida na watalii wameruhusiwa kurudi eneo hilo.
Via>>BBC
Social Plugin