Watu watano akiwemo mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi John Dotto na mbunge wa Nyamagana Mkoani Mwanza Stanslaus Mabula wamenusurika kifo baada ya kupata ajali eneo la Dumila mkoani Morogoro.
Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo imehusisha gari lao kugongana na Trekta lililokuwa likingia bila tahadhari barabara kuu .
Majeruhi hao wamelazwa katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.
Chanzo: Mwandishi wa ITV Morogoro Vedasto Msungu
Tutawaletea taarifa kamili hivi punde
Social Plugin