Suala la mipaka ya kimataifa mara nyingi huchukuliwa kama la kisiasa zaidi ya kitamaduni ambapo watu huwa na utaratibu wa kuivuka kihalali au kwa njia za panya. Baadhi ya mipaka inayozigawa nchi duniani huwa rahisi baina ya mataifa, wakati mwingine huwa na uzio, patrols, na vitisho vya vifo au kifungo kwa wasioiheshimu.
Worldatlas imetoa orodha ya nchi 10 zilizopakana na nchi nyingi zaidi huku China ikitajwa kuwa na majirani wengi zaidi kwa kuziweka Macau na Hong Kong kama nchi zinazojitegemea licha ya hini ya mamlaka ya China.
10: Turkey – imepakana na nchi nane
Turkey ina-share eneo la pekee katika ramani ya dunia, ikiwa na eneo la kilomita za mraba 756,816 Asia Magharibi (Anatolia) na ardhi ya kilomita za mraba 23,764 Kusini-mashariki ya Europe (Thrace).
Inapakana na nchi nyingi za Europe na Asia na Bahari Nyeusi upande wa kaskazini, kaskazini-mashariki inapakana na Armenia na Georgia, mashariki inapakana na Azerbaijan na Iran, magharibi na kusini-magharibi inapakana na Mediterranean Sea, kusini-mashariki inapakana na Iran na Syria, na kaskazini-magharibi inapakana na Ugiriki na Bulgaria.
9: Tanzania – inapakana na nchi 8
Nchi ya Afrika Mashariki Tanzania ina majirani wanane zikiwemo nchi za Kenya na Uganda upande wa kaskazini, Mozambique, Malawi na Zambia upande wa kusini, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa magharibi.
8: Serbia – inapakana na nchi nane
Serbia, nchi iliyopo Kusini-mashariki ya Balkan Peninsula barani Ulaya ni nchi ambayo inapakana na nchi nane pia. Inapakana na Hungary, Bulgaria, Romania, Macedonia, Montenegro, Croatia, Bosnia na Herzegovina.
7: Austria – inapakana na nchi nane
Austria ni nchi inapakana na Jamhuri ya Czech na kaskazini-mashariki inapakana na Slovakia. Mashariki inapakana na Hungary na Slovenia upande wa kusini huku Italy ikiwa upande wa kusini-magharibi. Switzerland na Liechtenstein zipo upande wa magharibi na Ujerumani upande wa kaskazini-magharibi.
6: Metropolitan France – inapakana na nchi nane
Ufaransa inapakana na Luxembourg na Ubelgiji na mashariki inapakana na Italy, Ujerumani na Switzerland, upande wa kusini inapakana na Uhispania na Andorra na kaskazini inapakana na England.
5: Ujerumani – inapakana na nchi tisa
Ujerumani inachangia mipaka yake na nchi 9 ambapo kaskazini inapakana na Denmark, magharibi inapakana na Netherlands, Luxembourg na Ubelgiji na kusini-magharibi kuna Ufaransa. Upande wa mpaka wa kusini inapakana na Austria na Switzerland. Kusiki-mashariki inapakana na Jamhuri ya Czech na mashariki zaidi kuna nchi ya Poland.
4: DR Congo – inapakana na nchi tisa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) inapakana na Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Congo, na Sudan. Mashariki inachangia mpaka na Burundi, Uganda, Tanzania na Rwanda huku Zambia ikiwa kusini-mashariki na Angola upande wa kusini-magharibi.
3: Brazil – inapakana na nchi 10
Brazil inachangia mipaka na nchi 10 za Amerika ya Kusini ambazo ni Argentina, Bolivia, Colombia, Venezuela, Uruguay, French Guyana, Paraguay, Guyana, Peru, na Suriname.
Mpaka wa Brazil na Argentina
2: Russia – inapakana na nchi 14
Ikiwa na mipaka inayofikia urefu wa kilomita 20,241 Russia ni nchi ya pili kwa kuwa na majirani wengi zaidi duniani ikipakana na nchi tofauti 14.
Kusini inachangia mipaka na nchi za Korea Kaskazini, Mongolia na China, Georgia, Kazakhstan, na Azerbaijan huku kusini-magharibi na magharibi inapakana na Ukraine, Estonia, Belarus, Latvia, Lithuania, Poland, Norway, na Finland.
Mpaka unaozitenganisha nchi tatu; Russia, China na North Korea
1: China – inapakana na nchi 16
Nchi ya pili kwa ukubwa wa eneo duniani, Jamhuri ya watu wa China inachangia mipaka ya kimataifa na nchi 16 ikiwemo Korea Kaskazini na Urusi upande wa kaskazini-mashariki na Mongolia upande wa kaskazini.
Upande wa kusini inapakana na Indian subcontinent inayojumuisha nchi za India, Bhutan, na Nepal. Vietnam, Laos, na Myanmar ziko upande wa kusini-mashariki na Pakistan upande wa kusini-magharibi.
Mipaka ya magharibi Afghanistan, Kazakhstan, Kyrgyzstan, na Tajikistan ambapo mbali na nchi hizi 14 inachangia mpaka na Macau na Hong Kong.
Mpaka baina ya China na Mongolia