Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Tazama Picha: CHAMA CHA WATU WENYE UALBINO CHATOA ELIMU MASUALA YA UALBINO KANISA KUU LA KKKT SHINYANGA


Chama cha watu wenye ualbino nchini (Tanzania Albinism Society-TAS) kimeanza kampeni ya kutoa elimu kuhusu masuala ya ualbino katika nyumba za ibada ambapo leo viongozi wa chama hicho taifa wametoa elimu katika kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria lililopo mjini Shinyanga.

Viongozi hao wakiongozwa na Afisa Mahusiano na Habari kutoka TAS ,Josephat Torner wametoa elimu kuhusu mambo ya ualbino kanisani hapo wakati wa ibada ya Jumapili leo Machi 26,2017.

Akizungumza kanisani hapo Torner alisema kampeni hiyo inalenga kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala ya ualbino kwa viongozi wa dini na waumini wao na wanaendelea pia kutoa elimu hiyo kwa makundi mengine ya watu katika jamii wakiwemo waganga wa kienyeji.

“Tumeona vita hii tunayopambana nayo bila kumjua hasa adui ni nani,ni vyema elimu iwafikie watu wengi zaidi na tunaamini kupitia nyumba za ibada jamii itakuwa na uelewa wa kutosha juu ya masuala ya ualbino ili kukabiliana na tatizo la mauaji ya watu wenye ualbino na hata vitendo vya kufukua makaburi ya watu wenye ualbino vinavyoendelea kujitokeza nchini”,alieleza Torner.

Alisema bado watu wengi hawana elimu ya kutosha kuhusu masuala ya ualbino hali inayosababisha kuongezeka kwa unyanyapaa ambapo sasa hata wamiliki wa nyumba za kupanga wanawanyima vyumba watu wenye ualbino wakihofia kupata matatizo.

“Nyumba za ibada zina watu wengi,tutapita kwenye makanisa na misikiti kutoa elimu hii ili viongozi na waumini waelewe hasa maana ya ualbino ili tuungane pamoja kutokomeza vitendo vya kikatili dhidi ya watu wenye ualbino”,aliongeza Torner.

“Kutokana na imani potofu katika jamii watu wenye ualbino wanaishi kwenye vituo maalum,wanaishi kwa hofu kubwa ya kuuawa na sasa kuna baadhi ya watu wameanza kufukua makaburi ya watu wenye ualbino hivyo kunahitajika jitihada zaidi katika kupambana na ukatili huu”,alisema Torner.

Alisema mbali na jitihada zinazofanywa na serikali katika mapambano dhidi ya ukatili huo ni vyema jamii ikatoa ushirikiano katika kupiga vita vitendo hivyo vya kikatili.

Akizungumza kwa niaba ya uongozi wa kanisa hilo,Mchungaji Jackson Maganga alisema kanisa hilo lina programu nyingi za kutoa elimu kwa waumini wake juu ya vitendo vya ukatili kwa watu wenye ualbino na kwamba kanisa hilo liko tayari kushirikiana na chama hicho katika mapambano dhidi ya ukatili kwa watu wenye ualbino.

Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo wakati wa ibada ya Jumapili katika kanisa hilo,ametusogezea picha 23 za matukio yaliyojiri..Tazama hapa chini
Mchungaji Geofrey Kaijunga akitoa mahubiri katika ibada ya Jumapili katika kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria lililopo mjini Shinyanga.
Mchungaji Geofrey Kaijunga aliwataka waumini wa kanisa hilo kumtegemea mungu kwa kila jambo huku akisisitiza kuwa thamani ya mtu hupanda pale anapookoka
Ibada ya Jumapili katika kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria ikiendelea
Mchungaji Jackson Maganga wa kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, akiwakaribisha kanisani viongozi wa chama cha watu wenye ualbino nchini Tanzania
Afisa Programu kutoka chama cha watu wenye ualbino Tanzania Severin Edward akiteta jambo na Afisa Mahusiano na habari kutoka chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS)Josephat Torner
Kushoto ni Mkurugenzi wa wanawake,Watoto na Diakonia katika kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Martha Ernest Ambarang'u akiwatambulisha viongozi kutoka TAS.Wa pili kutoka kushoto ni Afisa Programu kutoka TAS Severin Edward ,akifuatiwa Happiness Ngaweje na afisa mahusiano na habari (TAS)Josephat Torner
Afisa Mahusiano na habari kutoka chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS) Josephat Torner akitoa elimu kuhusu masuala ya ualbino katika kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria

Afisa Mahusiano na Habari kutoka TAS,Josephat Torner akizungumza kanisani
Waumini wakimsikiliza Afisa Mahusiano na habari kutoka chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS) Josephat Torner


Afisa Mahusiano na habari kutoka chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS) Josephat Torner akiendelea kutoa elimu kuhusu masuala ya ualbino huku akiitaka jamii kutoa ushirikiano wa dhati katika mapambano dhidi ya ukatili kwa watu wenye ualbino
Afisa Mahusiano na habari kutoka chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS) Josephat Torner akizungumza kanisani
Waumini wakipa somo kuhusu masuala ya ualbino
Mchungaji Jackson Maganga wa kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria akieleza namna kanisa hilo linashiriki katika mapambano dhidi ya ukatili kwa watu wenye ualbino
Mchungaji Jackson Maganga akizungumza kanisani
Waumini wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea kanisani
Mchungaji Goodluck Mosha akizungumza jambo kanisani
Wachungaji wa kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria 
Viongozi wa TAS wakiwa kanisani
Waumini wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea kanisani
Waumini wa kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria wakiwa nje ya kanisa baada ya ibada kumalizika
Viongozi wa TAS wakiondoka katika kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria 
Kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com