Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha 20: AIRTEL YAZINDUA DUKA LA HUDUMA KWA WATEJA SHINYANGA MJINI



Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imezindua Duka la Huduma ya wateja mjini Shinyanga kwa lengo la kurahisha huduma zinazotolewa na kampuni hiyo kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga.

Mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa duka hilo la huduma kwa wateja lililopo karibu na uwanja wa Shycom mjini Shinyanga alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro.

Awali akizungumza wakati wa kuzindua duka hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel nchini Sunil Colaso alisema wamezindua duka hilo ili kuongeza wigo wa soko mkoani Shinyanga na kuwasogezea huduma wananchi.

“Tunafuraha kubwa kufungua duka hili leo ambalo ni miongoni mwa maduka sita ambayo yanafunguliwa mkoani Shinyanga,hili ni duka la pili Mjini Shinyanga na tunatarajia kufungua maduka mengine ndani ya mwezi huu”,alieleza Colaso.

Aidha Colaso alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wakazi wa Shinyanga kufika katika duka hilo la huduma kwa wateja ili kupata huduma mbalimbali ikiwemo kurudisha namba zilizopotea,kuuza laini,simu,kurekebisha namba za siri za Airtel Money na huduma nyinginezo.

Naye mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro  alisema uwepo wa duka hilo utaongeza ajira kwa vijana na pia itarahisisha upatikanaji wa huduma muhimu za simu kwa wananchi ikiwemo huduma za pesa.

“Yanapofunguliwa maduka mengi inasaidia kupunguza umbali wa wananchi kufuata huduma,nawaomba wananchi kila mtu asajili simu yake kwa majina yake halisi ili kupunguza vitendo vya uhalifu",alisema Matiro.

“Nawaomba wananchi mtumie maduka haya kupata huduma mnazohitaji badala ya kutumia watu wa kati ambao baadhi yao siyo waaminifu,kumbukeni mawasiliano ni maendeleo,bila mawasiliano maendeleo yanakuwa ni shida,na sisi tunapoangalia vipaumbele vya maendeleo huwa tunaangalia pia kuna mawasiliano gani”,aliongeza Matiro.

Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo wakati za uzinduzi wa duka la huduma kwa wateja mjini Shinyanga,ametuletea picha 20 za matukio yaliyojiri
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania bwana Sunil Colaso akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro katika duka la huduma kwa wateja wakati wa uzinduzi wa duka hilo lililopo katika mtaa wa Buzuka karibu na uwanja wa Shycom mjini Shinyanga leo Jumanne Machi 14,2017 
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania bwana Sunil Colaso akiteta jambo na mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro wakati wa uzinduzi wa duka la huduma kwa wateja
Meneja wa kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania Kanda ya Kati bwana Stephen Akyoo akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka la huduma kwa wateja mjini Shinyanga 
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania bwana Sunil Colaso akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka la huduma kwa wateja mjini Shinyanga
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania bwana Sunil Colaso akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma kwa wateja.Katikati ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro na Afisa mtendaji wa kata ya Shinyanga Mjini Simon Mashishanga wakimsikiliza mkurugenzi huyo wa Airtel
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka la huduma kwa wateja
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka la huduma kwa wateja.Kulia ni Mawakala wa huduma za Airtel Money wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akikata utepe wakati wa uzinduzi wa duka la huduma kwa wateja.Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania bwana Sunil Colaso 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka la huduma kwa wateja la Airtel mjini Shinyanga
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania bwana Sunil Colaso akifurahia baada ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kukata utepe
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa ameshikilia boksi lenye simu zinazouzwa kwa bei nafuu katika duka la huduma kwa wateja
Meneja Mauzo wa Airtel mkoa wa Shinyanga James Moilo akitoa maelezo kwa mkuu wa wilaya Josephine Matiro kuhusu huduma zinazotolewa katika duka hilo la huduma kwa wateja ambazo ni pamoja na kuuza simu,kurudisha namba zilizopotea,kubadili pin za Airtel Money n.k
Meneja Mauzo wa Airtel mkoa wa Shinyanga James Moilo akitoa maelezo kwa mkuu wa wilaya Josephine Matiro kuhusu simu za bei nafuu zinazouzwa katika duka hilo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa ndani ya duka la huduma kwa wateja
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwashukuru viongozi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kwa kufungua maduka ya huduma kwa wateja mkoani Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia simu ya kisasa 'Smartphone' katika duka la huduma kwa wateja mjini Shinyanga
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania bwana Sunil Colaso akiwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro katika duka la huduma kwa wateja
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akiagana na Meneja wa kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania Kanda ya Kati bwana Stephen Akyoo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akiagana na Meneja Mauzo wa kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania mkoa wa Shinyanga James Moilo 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akiwaaga mawakala wa huduma ya Airtel Money waliohudhuria uzinduzi wa duka la huduma kwa wateja.

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com