Askari wa kikosi cha kuzuia ghasia (FFU) mkoa wa Simiyu wakiwakamata baadhi ya wanafunzi wakati wa maandamano ya wanafunzi wa shule ya sekondari Bariadi iliyoko Bariadi mkoani Simiyu-Picha zote kwa hisani ya Simiyu News blog
Wanafunzi wa shule ya sekondari Bariadi iliyoko Bariadi mkoani Simiyu wakiandamana katikati ya barabara kuu ya Bariadi-Lamadi, mjini Bariadi wakishinikiza kurudishwa Mkuu wa shule yao ambaye alikuwa amepewa uhamisho Deus Toga, ambapo alikuwa amepelekwa shule ya sekondari Giriku na kuletewa Mkuu wa shule mwingine Paul Lutema ambaye walimkataa.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Bariadi wakiandamana katikati ya barabara kuu ya Bariadi-Lamadi
Askari wa kikosi cha kuzuia ghasia (FFU) mkoa wa Simiyu wakiwakamata baadhi ya wanafunzi wakati wa maandamano hayo
Askari wa kikosi cha kuzuia ghasia (FFU) mkoa wa Simiyu wakiwakamata baadhi ya wanafunzi wakati wa maandamano hayo.
Askari wa kikosi cha kuzuia ghasia (FFU) mkoa wa Simiyu wakimkamata mmoja wa wanafunzi wakati wa maanadamano hayo, ambapo walimkamata na kumuweka kwenye gari la polisi.
Askari wengine akimkimbiza mwanafunzi ili kumkamata
Akari wa kikosi cha kuzuia ghasia (FFU) mkoa wa Simiyu wakiwa katika eneo la shule ya sekondari Bariadi, kuhakikisha wanafunzi wanaingia darasani ili wasiendeleze maandamano.
Walimu wa shule ya sekondari Bariadi iliyoko Mjini Bariadi Mkoani Simiyu, wakiwatuliza wanafunzi wa shule hiyo wasiandamane tena, baada ya kurudishwa na askari wa FFU kwa mabomu ya machozi kutoka katikati ya barabara kuu ya Bariadi-Lamadi walipokuwa wakiandamana kwenda ofisi ya mkuu wa mkoa wa Simiyu kwa ajili ya kupinga uhamisho wa Mkuu wao wa shule.
Mwanafunzi akiwa amebebwa na wenzake baada ya kupoteza fahamu kutokana na kupigwa na mabomu ya machozi, wakati wakiwa katika maandamano kwenda ofisi ya mkuu wa mkoa wa Simiyu kwa ajili ya kupinga uhamisho wa Mkuu wao wa shule.
Mwanafunzi akiwa amepoteza fahamu
Wanafunzi wakiwa wamebeba mabango
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga, akiangalia mabango yaliyokuwa yamebebwa na wanafunzi hao, alipofika shuleni hapo kwa ajili ya kuwatuliza, na kusikiliza madai yao na kuamua mwalimu huyo kurejeshwa shuleni hapo.
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga, akiangalia mabango yaliyokuwa yamebebwa na wanafunzi hao
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga akiwatuliza wanafunzi hao
Wanafunzi hao wakiwa wanaandamana, barabara kuu ya bariadi-Lamadi
****
ZAIDI ya Wanafunzi 600 wa shule ya sekondari ya Bariadi iliyopo katika halmashauri ya mji wa Bariadi Mkoani Simiyu wameandamana na kufunga barabara kuu ya Bariadi –Lamadi kupinga kuhamishwa kwa mkuu wa shule hiyo Deus Toga.
Wanafunzi hao walianza kuandamana kwenda katika ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri,lakini ilishindikana baada ya kikosi cha jeshi la polisi kuzuia ghasia (FFU) kuwazuia kwenda katika ofisi hizo.
Hata hivyo wanafunzi hao wakiwa katikati ya barabara hiyo waliamua kuandamana tena kuelekea katika ofisi ya mkuu wa mkoa jambo lililoshindikana pia baada ya askari hao kuwazuia tena eneo la Hospitali teule ya mkoa (Somanda).
Baada ya hali hiyo wanafunzi hao ambao ni kidato cha kwanza hadi cha sita waliamua kukaa katikati ya barabara huku wakiimbanyimbo za kushinikiza kuwa hawamtaki mwalimu Paul Lutema ambaye alikuwa amepelekwa kuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo.
“Hatumtaki mwalimu Lutema……tunamtaka mwalimu wetu Toga…..hatumtaki Lutema……Tunamtaka mwalimu Toga”
Wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali za kumkataa mwalimu Lutema na kumtaka mwalimu Deus Toga wanafunzi hao walianza kuwarushia mawe askari hao wakitaka wasiwazuie kwenda ofisi ya mkuu wa mkoa.
Baada ya hali hiyo askari wa jeshi la polisi walianza kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanafunzi hao huku wakiwafukuza kurejea katika eneo la shule ambapo baadhi yao walikamatwa na kupigwa virungu na kuwekwa ndani ya magari ya polisi hadi kupelekwa kituo cha polisi Bariadi huku wengine wakipoteza fahamu.
“Tangu mwalimu huyu kafika shuleni hapa ufauru umeongezeka na migogoro ya shule iliyokuwepo haipo tena,na duka la shule lilikuwa limefungwa kutokana na migogoro ya walimu lakini toka amekuja hiyo migogoro imekwisha na duka linafanya kazi’’,alisema Justine Mshana.
Hata hivyo Kaimu Mkuu wa mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga alifika katika shule hiyo na kusikiliza madai yao na kuamua mwalimu huyo kurejeshwa shuleni hapo.