Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha: BASI LA RUKSA CLASSIC LAGONGANA USO KWA USO NA GARI DOGO SHINYANGA

Basi la RUKSA CLASSIC lenye namba za usajiri T636AWC likitoka jijini Mwanza kwenda mkoani Kigoma limegongana uso kwa uso na gari dogo lenye namba za usajiri T 210 DJJ katika kijiji cha Nhelegani  mkabala na chuo cha Ushirika Moshi kambi ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga.


Chanzo cha ajali hiyo  iliyotokea majira ya nne asubuhi inaelezwa kuwa  ni uzembe wa dereva wa gari ndogo ambaye hakuwa na utulivu barabarani na kujikuta yupo upande usio sahihi na kusababisha ajali.

Hata hivyo hakuna mtu aliyepoteza maisha ingawa dereva wa gari dogo na abiria wake mmoja, wameumia na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga.

Mwandishi mkuu wa MASENGWA BLOG Isaac Luhende alifika eneo la tukio mapema kabisa na ametuletea picha za tukio hilo
Basi likiwa limegongana  uso kwa uso na gari dogo
Basi la RUKSA CLASSIC
Gari dogo likiwa limefunikwa
Basi hilo 

Mbele ya basi
Watu wakisaidia kuichomoa gari hiyo
Gari dogo likiwa limeharibika
Watu wakishuhudia tukio hilo
Nyuma ya gari dogo












PICHA ZOTE KWA HISANI YA MASENGWA BLOG

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com