Wanawake wanaofanya kazi katika Mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu uliopo katika halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wameadhimisha siku ya wanawake duniani Machi 8,2017 kwa kutoa zawadi ya baiskeli kwa wanafunzi wa shule za sekondari pamoja na kuwatembelea na kuwapatia zawadi wagonjwa waliolazwa kwenye vituo vya afya.
Wanawake hao wametoa zawadi ya baiskeli 10 zikiwemo 8 kwa ajili ya wanafunzi waliofanya vyema katika masomo yao katika shule ya Sekondari Bulyanhulu na Bugarama na baiskeli mbili kwa ajili ya walimu wa kike walezi wa wanafunzi hao.
Mbali na kutoa zawadi kwa wanafunzi,pia wametembelea kituo cha afya cha Bugarama na Lunguya vilivyopo jirani na mgodi huo kisha kutoa zawadi ya shuka 70 kila kituo na kuwapa wauguzi na wagonjwa sabuni,mafuta ya kujipaka na dawa za meno vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 12.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ya siku ya wanawake,Afisa Uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo alisema wameamua kusherehekea siku hiyo muhimu kwa kuwapongeza wanafunzi wanaofanya vizuri shuleni ili kuwapa ari ya kujifunza zaidi na kuwarahisishia usafiri kufika shuleni.
“Tuwatembelea wanafunzi wa shule ya sekondari Bulyanhulu na Bugarama,tumetoa msaada wa baiskeli 10 hivyo kila shule imepata tano ambapo nne kwa ajili ya wanafunzi kike na moja ni kwa ajili ya walimu wa kike kwa kila shule”,alieleza Senkondo.
“Pia tumetoa shuka 140 kwa ajili ya vituo vya afya viwili,Bugarama na Lunguya kisha kugawa sabuni,mafuta na dawa za meno kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa waliopo katika vituo hivyo”,aliongeza Senkondo.
Senkondo alisema wameamua kushiriki maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kwa kukutana na watoto wa kike na wanawake ili kuwahamisha wanawake katika jamii kushiriki katika shughuli za migodi kwani wanaweza.
Mwandishi wetu Kadama Malunde,alikuwepo wakati wa maadhimisho hayo,ametuletea picha za matukio yaliyojiri mwanzo hadi mwisho…Tazama hapa chini
Wanafunzi wa shule ya sekondari Bulyanhulu wakiwa katika shule hiyo iliyopo katika kata ya Kakola halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga wakisubiri kupata zawadi kutoka kwa wanawake wanaofanya kazi katika mgodi wa Acacia dhahabu wa Bulyanhulu uliopo jirani na shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 920 wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
Afisa Uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo akizungumza wakati wa kukabidhi baiskeli nne kwa ajili ya wanafunzi wa kike waliofanya vyema katika mitihani yao ili ziwasaidie kurahisisha usafiri kufika shuleni lakini pia baiskeli moja kwa ajili ya mwalimu mlezi wa wanafunzi katika shule hiyo
Kulia ni Afisa Uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo akikabidhi baiskeli kwa mwalimu mlezi wa wanafunzi katika shule ya sekondari Bulyanhulu ,mwalimu Bumi Mwasalujonja
Mwalimu Bumi Mwasalujonja akiwa amebeba juu baiskeli wakati akikabidhiwa na wanawake kutoka mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu
Afisa Uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo akikabidhi baiskeli kwa mwanafunzi wa kidato cha tatu Irene Gimi aliyefanya vizuri katika mtihani wa kidato cha pili mwaka 2016 baada ya kupata daraja la kwanza
Mwanafunzi wa kidato cha tatu Irene Gimi akiondoka na baiskeli yake
Afisa Uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo akishikana mkono na mwanafunzi wa kidato cha tatu Zainab Kisambale aliyepata daraja la pili katika mtihani wa kidato cha pili mwaka 2016 na anaongea kwa ufasaha zaidi lugha ya Kiingereza
Wanawake kutoka mgodi wa Bulyanhulu akiwa na wanafunzi wanne waliofanya vizuri katika mtihani
Hapa ni katika shule ya Sekondari Bugarama iliyopo kata ya Bugarama ambayo imejengwa na mgodi wa Acacia Bulyanhulu.Katika shule hii pia wanafunzi wanne wa kike waliofanya vizuri katika masomo yao walipata zawadi ya baiskeli,huku mwalimu wa nidhamu naye akipata zawadi ya baiskeli
Afisa Uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo akikabidh baiskeli kwa mwalimu wa nidhamu/mlezi shule ya sekondari Bugarama Prisca Mwanantemi
Wanawake wanaofanya kazi katika mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakikabidhi baiskeli kwa mwalimu Prisca Mwanantemi
Afisa Uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo akimtambulisha mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule hiyo Jesca Peter ambaye hivi karibuni alifanya vizuri katika mtihani wa majaribio. Mwanafunzi huyo amepata zawadi ya baiskeli
Wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao pamoja na mwalimu wao wakiwa wameshikilia baiskeli zao
Wafanyakazi wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakiondoka katika shule ya sekondari Bugarama yenye jumla ya wanafunzi 766
Hapa ni katika Kituo cha afya Bugarama kilichopo katikakata ya Bugarama halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama.Kituo hiki cha afya kimepewa shuka 70 kwa ajili ya wagonjwa.Kulia ni Muuguzi katika kituo hicho Mwalushani Mabula akizungumza wakati wa kupokea shuka 70,sabuni,mafuta ya kujipaka na dawa za meno kwa ajili ya wagonjwa waliokutwa katika kituo hicho siku ya siku ya wanawake duniani Machi 8,2017
Wa pili kutoka kushoto ni Afisa Uhusiano wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Zuwena Senkondo akizungumza wakati wa kukabidhi shuka 70 kwa ajili ya wagonjwa lakini pia sabuni,dawa za meno na mafuta ya kujipaka kwa ajili ya wauguzi na wagonjwa katika kituo hicho cha afya
Afisa Uhusiano wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Zuwena Senkondo akikabidhi shuka kwa Muuguzi kituo cha afya Bugarama Mwalushani Mabula
Wanawake kutoka mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakikabidhi shuka kwa wauguzi wa kituo cha afya Bugarama
Zoezi la kugawa shuka likiendelea. Kituo cha afya Bugarama kimejengwa na mgodi wa Acacia Bulyanhulu
Wanawake kutoka mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakielekea katika wodi za wagonjwa kwa ajili ya kuwapatia zawadi ya sabuni,mafuta ya kujipaka na dawa za meno
Afisa Uhusiano wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Zuwena Senkondo akiwa katika wodi ya wazazi akiwaeleza akina mama waliojifungua kuwa wameamua kuwatembelea ili washerehekee kwa pamoja katika siku ya wanawake duniani kwa kuwapatia msaada
Afisa Uhusiano wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Zuwena Senkondo akitoa zawadi ya sabuni kwa Tedy Paul
Wafanyakazi wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakiwa wamebeba mtoto aliyezaliwa na Salome Raphael baada ya kumpatia zawadi ya vipande 10 vya sabuni,mafuta ya kujipaka na dawa ya meno
Zoezi la kugawa zawadi wodini likiendelea,ambapo kila mgonjwa alipewa vipande 10 vya sabuni,mafuta ya kupaka na dawa ya meno
Ndani ya wodi ya wazazi baada ya kumaliza kutoa sabuni,dawa za meno na mafuta ya kujipaka
Wanawake wanaofanya kazi katika mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakifurahia baada ya kutembelea kituo cha afya Bugarama
Wanaendelea kufurahia
Picha eneo la kituo cha afya Bugarama baada ya kutoa zawadi kwa wagonjwa
Hapa ni katika kituo cha afya Lunguya ambapo pia wanawake kutoka mgodi wa Acacia Bulyanhulu walitoa zawadi ya shuka 70,sabuni,mafuta na dawa za meno kwa ajili ya wagonjwa katika kituo hicho cha afya. Kulia ni Afisa Uhusiano wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Zuwena Senkondo akizungumza katika kituo hicho
Afisa Uhusiano wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Zuwena Senkondo akizungumza kabla ya kutoa zawadi hizo.Kulia ni wauguzi katika kituo hicho
Afisa Uhusiano wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Zuwena Senkondo akikabidhi shuka kwa Afisa tabibu wa kituo cha afya Lunguya,Dkt. John Malongo kwa ajili ya wagonjwa katika kituo hicho
Afisa Uhusiano wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Zuwena Senkondo akikabidhi shuka kwa wauguzi wa kituo cha afya Lunguya
Akina mama kutoka mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakigawa sabuni,mafuta na dawa za meno kwa akina mama ndani wodi ya watoto
Ugawaji wa zawadi unaendelea
Mama akifurahia baada ya kupata zawadi ya sabuni,dawa ya meno na mafuta ya kujipaka
Wanawake wanaofanya kazi katika mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakielekea katika wodi nyingine ya wagonjwa
Wanawake kutoka mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakimpatia zawadi mama aliyelazwa katika wodi ya akina mama
Zoezi la kugawa zawadi likiendelea
Mwanamme anayeuguza mama yake mzazi wodini naye akapewa zawadi ya sabuni,mafuta ya kujipaka na dawa ya meno
Kulia ni Afisa tabibu wa kituo cha afya Lunguya,Dkt. John Malongo akiwaaga wanawake kutoka mgodi wa Acacia Bulyanhulu
Wanawake wanaofanya kazi katika mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakiondoka katika kituo cha afya Lunguya
Wanawake wanaofanya kazi katika mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakiondoka katika kituo cha afya Lunguya baada ya kumaliza kutoa zawadi kwa akina mama na akina baba waliokuwa katika kituo hicho wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Picha 43: USIKU WA WANAWAKE WANAOFANYA KAZI MGODI WA DHAHABU ACACIA BULYANHULU KAHAMA
Picha 43: USIKU WA WANAWAKE WANAOFANYA KAZI MGODI WA DHAHABU ACACIA BULYANHULU KAHAMA
Social Plugin