RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AZINDUA TAASISI YAKE YA KUSAIDIA JAMII DUNIANI


Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (kulia), akizungumza alipokuwa akizindua rasmi Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) ikiwa ni sehemu pia ya uzinduzi wa taasisi hiyo kwenye Hotel ya Hyatt Kempinsk The Kilimanjaro Dar es Salaam jana. Kikwete ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo.


Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Jakaya Kikwete, alisema kuwa Taasisi hiyo pamoja na mambo mengine itajihusisha na masuala ya Maendeleo ya Binadamu nchini, Afrika na Duniani.


Kikwete akizungumza na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi yake ya JMKF


Jakaya Kikwete akikumbatiana na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi hiyo, Balozi wa zamani wa Marekani nchini Tanzania, Charles Stith


Mwenyekiti wa Taasisi ya JMKF, Jakaya Kikwete akisalimiana na mjumbe wa Bodi hiyo, Mfanyabiashara maarufu Mtanzania aishie Marekani, Genevieve Sangudi


Mwenyekiti wa Taasisi ya JMKF, Jakaya Kikwete akisalimiana na mjumbe wa Bodi hiyo ya Wadhamini , Dato' Sri Idris Jala, Waziri asiye na Wizara Maalumu Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia na Mtendaji Mkuu wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Pamendu) nchini humo.


Mwenyekiti wa JMKF, Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Taasisi hiyo.


Jakaya akijadiliana jambo na Balozi Charles Stith


Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi wa Taasisi hiyo.


Jakaya Kikwete akifafanua mambo mbalimbali kuhusu Taasisi hiyo




Dato' Sri Idris Jala kutoka Malaysia


Genevieve Sangudi kutoka Marekani


Mwanasheria Maarufu nchini, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar. Alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza 2006 na Marekani 2013




Daktari Bingwa wa Upasuasi, Profesa Wiliam Mahalu


Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandara


Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Makampuni la SS Bakhresa, Abubakar Bakhresa


Balozi wa zamani wa Marekani nchini, Charles Stith


Na Immaculate Makilika- MAELEZO
Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete amezindua Taasisi yake ya kusaidia jamii, nakusema ameamua kuanzisha taaisi hiyo ili kuwa na chombo kitakachomsaidia kuendeleza maono yake ya kutimiza ndoto zake katika kuendelea kusaidia jamii.

Akizindua taasisi hiyo yenye jila la Jakaya Mrisho Kikwete Foundation, Kikwete amesema, kwa muda mrefu amekua akipenda na kujihusisha na shughuli mbalimbali za maendeleo ya watu na hivyo taasisi yake itamsaidia katika kufikia malengo yake.

“Nimetumia muda wangu kwa ajili ya maendeleo ya watu, baada ya shule, nilikitumikia Chama cha Mapinduzi (CCM), nilitumikia Jeshi na baadae Serikali, kwangu Taasisi hii imekuwa chombo kitakachonisaidia kuendeleza maono yangu na kutimiza ndoto zangu katika kuendelea kusaidia watu” alisema Dk. Kikwete.

Akizungumzia taasisi hiyo Kikwete amesema ni taasisi yenye wajumbe tisa kutoka sehemu mbalimbali duniani wenye nyadhifa na heshima kubwa katika nchi zao.

Dk. Kikwete amewataja Wajumbe wa Bodi ya Udhamini ya Taasisi yake kuwa ni Balozi Ombeni Sefue aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Profesa Rwekaza Mukandala, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Willium Mahalu Mhadhiri Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Tabibu cha Bugando.

Wengine ni Balozi Mwanaidi Maajar aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Abubakar Bakhresa, Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa, Genevieve Sangudi Mtaalamu wa Masuala ya kibishara ya Kimataifa kutoka Marekani.

Aliwataja wengine kuwa ni Dato’ Sri Idris Jala, Waziri asiyekuwa na Wizara Maalumu nchini Malyasia, Balozi Charles R. Stith aliyekuwa Balozi wa zamani wa Marekani nchini Tanzania pamoja na Dkt. Carlos Lopes ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taaisi ya Mafunzo na Utafiti ya Umoja wa Mataifa (UNITAR).

Amesema taasisi hiyo inajikita kusaidia jamii katika maeneo makubwa manne ya maendeleo ya jamii ikiwemo kuondoa umaskini, mabadiliko ya tabia nchi, kilimo kwa wakulima wadogo, huduma za afya ikiwemo kutokomeza malaria na afya ya mama na mtoto.

Maeneo mengine ameyataja taasisi hiyo kushughulika nayo ni elimu kwa vijana ili kukuza vipaji vyao na kuwapa mafunzo kuhusu uongozi bora, usawa wa kijinsia na namna ambavyo Serikali inavyotoa huduma kwa wananchi.

Amesisitiza kuwa taasisi yake itaisaidia Serikali, mashirika na taasisi mbalimbali ili kushirikiana kuwaletea maendeleo Watanzania na watu mbalimbali duniani.

Taasisi ya Maendeleo ya Jakaya Kikwete ilisajiliwa tarehe 17, Februari 2017, na hii ni mara ya kwanza kwa wajumbe wa bodi ya wadhamini kukutana tangu kuanzishwa kwake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post