Rais wa Marekani Donald Trump ametaka bunge la Congress kuchunguza ikiwa Barack Obama alitumia vibaya mamlaka yake wakati wa kampeni ya uchaguzi siku moja baada ya kudai kuwa Obama alikuwa akidukua simu zake.
Msemaji wa Trump alisema kwa uchunguzi kuhusu kuingia kwa Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani utasaidia uchunguzi huo.
Trump alitoa madai hayo kwenye mtandao wa tittwer lakini hakutoa ushahidi wowote.
Aliyekuwa mkuu wa ujasusi nchini Marekani James Clapper, wakati wa kampeni alikana kuwa mawasiliano kwenye jumba la Trump Tower hayakunakiliwa.
Msemaji wa Obama Kevin Lewis, alisema kuwa rais huyo wa zamani hakuwai amrisha kudukuliwa kwa raia yeyote wa Marekani.
Trump ambaye anakabiliana na uchunguzi mkubwa unaohusu Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani, alitoa madai hayo kupitia mtandoa wa twitter akiwa jimbo la la Florida siku ya Jumamosi.
Chanzo-BBC
Social Plugin