Shirika la afya Uingereza “NHS” limesema hivi karibuni wataanza kutumia Mbwa kugundua saratani ya tezi dume ambayo huwaathiri zaidi wanaume kuanzia miaka 50.
Kwa mujibu wa utafiti kwa zaidi ya asilimia 93 mbwa huweza kugundua cancer hiyo kwa kunusa mkojo wa mtu anayeugua saratani hiyo.
Akizungumza na CNN mbunge Jeremy Hunt alisema……. >>>‘ni vizuri kuangalia na njia zingine katika kufanya mambo na si lazima kila muda kutegemea sayansi na wataendelea kuangalia usahihi wa mbwa katika kugundua saratani hiyo na kuipa nafasi’.
Kutumika kwa mbwa katika kugundua magonjwa mbalimbali si jambo geni ambapo mwaka 2016 ili ripotiwa Mtoto wa miaka wa 13 kutumia Mbwa wake kugundua ugonjwa wa kisukari na mwaka 2009 Mbwa alitumika kugundua saratani ya matiti.