Askofu mkuu wa kanisa la AICT Silas Kezakubi-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog |
Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) limechukua uamuzi mgumu leo Jumapili Aprili 2,2017 ambapo askofu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga Dkt. John Kanoni Nkola amestaafishwa leo huku askofu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Mwanza John Bunangwa akitakiwa kujiuzulu kwa kushindwa kusimamia vizuri fedha za mkopo kwa ajili ya shule ya kanisa hilo.
Kanisa hilo pia limevua uchungaji wachungaji watatu wa kanisa hilo ambao ni Emmanuel Isaya,Dkt Meshack Kulwa na Jakobo Mapambano aliyekuwa katibu mkuu wa kanisa hilo dayosisi ya Shinyanga.
Msikilize hapa Askofu mkuu wa kanisa la AICT Silas Kezakubi akitangaza uamuzi wa baraza la utendaji sinodi kuu kanisa la AICT leo katika kanisa la AICT Kambarage mjini Shinyanga.
SIKILIZA HAPA CHINI
Social Plugin