BUNGE limearifiwa kuwa kwa sasa nchi haina tatizo la upungufu wa dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi (ARVs).
Kauli hiyo ilitolewa bungeni na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Fatma Toufiq (CCM) aliyetaka kufahamu mpango wa serikali wa kuwa na kiwanda cha kutengeneza ARVs.
Waziri Ummy alisema kuhusu dawa za ARVs zinazoingizwa nchini, kuna dawa za watoto ambazo ni pamoja na Nevirapine Syrup na Lopinavir/Ritonavir Syrup.
Alisema dawa nyingine ni pamoja na mchanganyiko wa dawa za vidonge mfano Lamivudine/Atazanavir/ Niveraphine (3TC/AZT/ NPV) zenye nguvu ya 30mg/60mg.
Alisema serikali inahamasisha mashirika, taasisi, wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji kuwekeza kwenye viwanda vya kuzalisha dawa mbalimbali zikiwemo ARVs.
Alisema kwa sasa kuna kiwanda mkoani Arusha cha TPI ARV Limited ambacho kimepewa leseni ya kutengeneza ARVs.
“Kiwanda hakijaanza uzalishaji, wizara inatarajia kiwanda hicho kitaanza uzalishaji wa ARVs hivi karibuni,” alisema Waziri Ummy.
Social Plugin