Furaha ni kitu ambacho kila mtu hukililia na hutamani kuwa nayo kila wakati na kila mahali na huwa ni jambo la kujivunia sana kuishi kwa furaha.
Leo Aprili 16, 2017, imenifikia stori hii ambayo ilichapishwa na CNN April 14, 2017 ambapo unaambiwa mji wa Dubai umeanzisha kampeni maalumu kwa ajili ya kuufanya mji huo kuwa wenye furaha zaidi duniani kwa kuanzisha kipimo maalum kujua hali ya furaha ya watu wake kiitwacho ‘Happiness Meters’.
Unaambiwa katika kila meter kuna emoji tatu – sura ya furaha, sura neutral na sura ya huzuni ambapo watu huzitumia kuelezea kuridhishwa au kutoridhishwa kwao na huduma za kila siku mjini humo.
Mkurugenzi Mkuu wa Smart Dubai aliiambia CNN: “Ili kuwa mji wenye furaha, tulijua tungalihitaji njia ya kuwasikiliza kila mmoja kwenye mji, na kuelewa kiwango chao cha sasa cha furaha kutokana na huduma za mji.” – Dr. Aisha Bin Bishr.
United Arabs Emirates ina Wizara maalum ya Furaha ambayo kazi yake ni kuipromoti na kiupa kipaumbele furaha katika serikali na maisha ya kila siku huku kukiwa na Wakurugenzi Wakuu Watendaji wa Furaha 60 katika Idara zote za Serikali.