Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Freemason Afrika Mashariki, Sir Jayantilal Keshavji Chande maarufu kama Andy Chande, umeteketezwa leo Kijitonyama, jijini Dar es Salaam kupitia tukio lililodumu kwa takribani saa moja.
Mwili huo umeteketezwa kwa moto kupitia ibada iliyofanyika kwenye nyumba maalumu inayotumika kama sehemu ya maziko ya waumini wa dini ya Hindu.
Sir Chande alifariki dunia siku tano zilizopita wakati akipata matibabu katika hospitali ya Nairobi baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa ulitokana na matatizo ya utumbo mdogo kusambaza sumu mwilini.
Social Plugin