Rushwa ni miongoni mwa vitu vinavorudisha nyuma maendeleo ya nchi nyingi duniani, hukwamisha maendeleo na kusababisha kukosekana kwa haki, utawala bora na uvunjifu wa sheria katika nchi nyingi duniani.
Licha ya kuwa rushwa ni tatizo kwa nchi nyingi duniani, lakini kuna nchi zinatajwa kuwa na kiwango kidogo cha rushwa huku sababu kubwa ikitajwa kuwepo kwa utawala bora, uwazi katika kufanya maamuzi na maendeleo ya kiuchumi .
Kwa mujibu wa Corruption Perception Index hizi ndizo nchi 10 zenye kiwango kidogo cha rushwa kwa mwaka 2017.
1: Denmark
Licha ya kuwa miongoni mwa nchi zenye furaha duniani, Denmark inatajwa pia kuwa nchi namba moja yenye kiwango kidogo cha rushwa ambapo kwa mujibu wa Corruption Perception Index nchi hiyo imeweza kupambana na rushwa kwa asilimia 92 kwa mwaka 2017.
2: New Zealand
Ni nchi namba mbili kuwa na kiwango kidogo cha rushwa duniani ambapo sababu kubwa inayofanya nchi hii kuwa na kiwango kidogo cha rushwa ni uwepo wa utawala bora. Serikali ya New Zealand hufanya maamuzi kwa uwazi na hali nzuri ya kiuchumi.
3: Finland
Miongoni mwa sababu inayoifanya Finland kuwa na kiwango kidogo cha rushwa kwa mujibu wa taasisi ya kuchunguza rushwa duniani ni uwepo wa hali ya haki na usawa na hali nzuri ya kiuchumi. Imepata 89%.
4: Sweden
Kwa mujibu wa Katiba ya Sweden, Bunge lina nafasi kubwa ya kufanya maamuzi ukilinganisha na serikali. Hali hii inaifanya serikali ya nchi hiyo kuogopa kufanya makosa ya rushwa kwa sababu ya Bunge kuwa na nguvu kubwa. Aidha, katika nchi hii matumizi mabaya ya madaraka huonekana pia kama rushwa.
5: Norway
Norway ni miongoni mwa nchi zenye kiwango kidogo cha rushwa, na kwa mujibu wa Corruption Perception Index, inapata 86% kwa kuweza kupambana na rushwa kwa mwaka 2017.
6: Switzerland
Switzerland imefanikiwa kupambana na rushwa kwa 86% na kwa mujibu wa taasisis ya kupambana na rushwa, nchi hiyo imefanikiwa kwa sababu Katiba yake inaruhusu wananchi kujihusisha katika majidiliano wakati serikali inafanya maamuzi kupitia njia ya kura za maoni.
7: Singapore
Kwa mujibu wa Corruption Perception Index, Singapore imefanikiwa kwa zaidi ya 84% kupambana na rushwa na inatajwa kuwa nchi ya saba kwa mwaka 2017 kuwa na kiwango kidogo cha rushwa.
8: Uholanzi
Uholanzi ni miongoni mwa nchi zinazotajwa na Corruption Perception Index kwa kuwa na kiwango kidogo cha rushwa ambapo sababu kubwa inayochangia ni uwepo wa program za kuzuia rushwa.
9: Luxembourg
Inatajwa kuwa moja kati ya nchi ndogo na tajiri zaidi katika nchi za Umoja wa Ulaya ambapo sababu kubwa inayoifanya nchi hiyo kuwa mongoni mwa nchi zenye kiwango kidogo cha rushwa ni hali ya uchumi kuwa nzuri kwa kila raia wa nchi hii.
10: Canada.
Canada ni miongoni mwa nchi zenye kiwango kidogo cha rushwa duniani ambapo moja ya sababu kubwa inayochangia kuwepo kwa kiwango kidogo cha rushwa ni Bunge la nchi hiyo kuwa na nguvu zaidi ya serikali hivyo kupelekea serikali kufanya maamuzi kwa uwazi na utawala bora.
Social Plugin