Picha 10: WANAFUNZI WA CHUO CHA VETA MOSHI WATEMBELEA BANDA LA MGODI WA BULYANHULU MAONESHO YA USALAMA NA AFYA KAZINI


Wanafunzi wanaosoma katika Chuo Cha Ufundi – VETA Moshi mkoani Kilimanjaro wanasomea kozi maalumu kuhusu ufundi wa mgodini na viwandani wametembelea banda la mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi kwenye maonesho ya wiki ya usalama na afya mahali pa kazi mwaka 2017. 

Wakiwa katika banda hilo wamejionea namna mgodi huo unavyozingatia masuala ya afya na usalama kwa wafanyakazi mgodini ili kujiepusha na magonjwa na ajali zinazoweza kutokea wakiwa kazini. 

Wanafunzi hao wanatoka katika vijiji vinavyozunguka mgodi wa Bulyanhulu uliopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga. 

Banda la Mgodi wa Bulyanhulu mwaka huu limetia for a kwa kutembelewa na wananchi,walimu,watalii kutoka nje ya nchi na wafanyakazi mbalimbali ambapo tangu Aprili 26,2017 mpaka leo Aprili 29,2017 zaidi ya watu 1200 wametembelea banda hilo.

Katikati ni Afisa Mahusiano Mgodi wa Bulyanhulu Mary Lupamba akielezea masuala ya afya na usalama mgodini kwa wanafunzi wanaosomeshwa na mgodi huo katika chuo cha VETA Moshi
Afisa Mahusiano Mgodi wa Bulyanhulu Mary Lupamba akisisitiza jambo kwa wanafunzi wanaosoma chuo cha Veta Moshi waliotembelea banda la mgodi huo
Wa pili kulia ni  Afisa Rasilimali Watu Mgodi wa Bulyanhulu Mwanaisha Mosha akiwakaribisha walimu kutoka chuo cha VETA Moshi walioambatana na wanafunzi wao.Wa kwanza kushoto ni  Mwalimu Esrom Lema akifuatiwa na mwalimu  Emmanuel Kweka aliyevaa fulana zilizotolewa na mgodi wa Bulyanhulu kwa ajili ya walimu wanaofundisha katika chuo hicho
Kushoto ni Afisa Mazingira Mgodi wa Bulyanhulu Digna Isdory na Afisa Rasilimali Watu Mgodi wa Bulyanhulu Mwanaisha Mosha wakizungumza na wanafunzi wa chuo cha VETA waliotembelea banda la mgodi huo
Afisa Rasilimali Watu Mgodi wa Bulyanhulu Mwanaisha Mosha akijiandaa kugawa fulana kwa wanafunzi 9 wanaosomeshwa na mgodi wa Bulyanhulu katika chuo cha VETA.
Wa pili kutoka kushoto ni  Afisa Mazingira Mgodi wa Bulyanhulu Digna Isdory akiendelea na zoezi la kugawa fulana kwa wanafunzi wanaosoma katika chuo cha VETA Moshi waliotembelea banda la mgodi huo
Wanafunzi wanaosoma katika chuo cha VETA Moshi waliotembelea banda la mgodi wa Bulyanhulu wakivaa fulana walizopewa na mgodi huo
Wanafunzi wa chuo cha VETA wakivaa fulana zilizotolewa na mgodi wa Bulyanhulu
Maafisa kutoka mgodi wa Bulyanhulu wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi 9 wanaosomeshwa na mgodi huo katika chuo cha VETA
Picha ya pamoja wanafunzi na maafisa kutoka mgodi wa Bulyanhulu
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post