Picha 26: VIONGOZI WILAYA YA MEATU,KISHAPU,IRAMBA NA IGUNGA WAFANYA KIKAO KUNUSURU ZIWA KITANGIRI


Ijumaa Aprili 7,2017 viongozi wa wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu,Iramba- Singida,Igunga-Tabora na Kishapu- Shinyanga wamekutana kujadili namna ya kunusuru ziwa Kitangiri ambalo lipo hatarini kupotea kutoka na shughuli za kibinadamu zinazofanyika kwenye vyanzo vya ziwa na ndani ya ziwa hilo ikiwemo kilimo na ufugaji.

Ziwa hilo linatajwa kuwa na matope kutokana na shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo na ufugaji.

Miongoni wa wajumbe wa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Jengo la Ukaguzi Hesabu za Serikali mkoa wa Shinyanga ni wakuu wa wilaya,wakurugenzi,kamati za ulinzi na usalama wilaya,madiwani,kamati za mipango na fedha na wataalamu mbalimbali kutoka katika wilaya hizo nne.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Mkurugenzi Msaidizi Rasilimali za Maji wizara ya maji na umwagiliaji Naomi Lupimo na Afisa Maji kutoka bodi ya Maji Bonde la kati Benard Chikarabhani.

Viongozi hao wamejadili namna ya kutengeneza uhifadhi na matumizi endelevu ya ziwa Kitangiri ambalo lipo katika mpaka wa mkoa wa Shinyanga,Simiyu,Singida na Tabora 

Ziwa Kitangiri linapokea maji kutoka mto Manonga,Sanga,Sibiti,Semu,Ndurumo na Nzalala.

Mwandishi wetu Kadama Malunde ametuletea picha 26 za matukio wakati wa kikao hicho
Mwenyekiti wa kikao cha ujirani mwema wilaya nne za Iramba,Meatu,Igunga na Kishapu kujadili ziwa Kitangiri ambaye ni mkuu wa wilaya ya Iramba Emmanuel Luhahula akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa 
Mwenyekiti wa kikao hicho mkuu wa wilaya ya Iramba Emmanuel Luhahula 
Wajumbe wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Wajumbe wakiwa ukumbini
Wajumbe wa kikao hicho wakiwa ukumbini
Kikao kinaendelea
Mkuu wa wilaya ya Meatu Dkt. Joseph Elieza Chilongani akielezea namna ya kunusuru ziwa Kitangiri 
Mkuu wa wilaya ya Igunga John Mwaipopo akichangia hoja ukumbini
Kikao kinaendelea
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba akichangia hoja ukumbini 
Diwani wa kata ya Tulya wilaya ya Iramba Wilfred Kizanga akielezea historia ya ziwa Kitangiri ambalo sasa maji yake yamepungua kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu zinazoendelea ziwani ikiwemo kilimo ,uvuvi haramu
Diwani wa kata ya Mwabuzo wilaya ya Meatu Chalya Seni akichangia hoja
Diwani wa kata ya Ntwike wilaya ya Iramba Albert Said Mwakwala 
Afisa Malisho wilaya ya Iramba Fredrick Mpinga akielezea kuhusu ziwa Kitangiri ambalo linapokea maji kutoka mto Manonga,Sanga na Semu 
Mjumbe akichangia hoja
Mkurugenzi Msaidizi Rasilimali za maji wizara ya maji na umwagiliaji Naomi Lupimo akielezea sheria mbalimbali zinazotekelezwa na wizara hiyo ambapo alisema panatakiwa kufanyika utafiti ili kujua maji yanaendelea kupungua kiasi gani ili kujua namna ya kulifanya ziwa liendelee kuwepo 
Mkurugenzi Msaidizi Rasilimali za maji wizara ya maji na umwagiliaji Naomi Lupimo alisema sheria zao juu ya usimamizi wa rasilimali za maji ni nzuri hivyo anaamini sheria zilizopo ni nzuri kinachotakiwa ni usimamizi wa sheria na kuongeza kuwa kuna umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi
Afisa Maji kutoka bodi ya Maji Bonde la kati Benard Chikarabhani akizungumza ukumbini ambapo alisema jambo la uhifadhi wa ziwa Kitangiri linahitaji ushirikiano ambapo wadau wote wanapaswa kuungana 
Mkuu wa polisi wilaya ya Iramba Hamis Waryoba akichangia hoja katika kikao hicho na kusisitiza kuwa suala ya ufugaji linachachangia kwa kiasi kikubwa kupotea kwa ziwa Kitangiri
Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba akiteta jambo na mkuu wa wilaya ya Iramba Emmanuel Luhahula
Afisa Uvuvi Mfawidhi kanda ya kati Charles Kalumbete akichangia hoja katika kikao hicho
Mwanasheria wilaya ya Meatu Said Kisamba akizungumza ukumbini
Mkurugenzi wa halmashauri yaa wilaya ya Kishapu Stephen Magoiga akichangia hoja kwenye kikao hicho
Mkuu wa wilaya ya Igunga John Mwaipopo akifunga kikao hicho
Mkuu wa wilaya ya Igunga John Mwaipopo akizungumza wakati wa kufunga kikao
Wajumbe wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post