Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WACHUNGAJI ZAIDI YA 300 WA MADHEHEBU MBALIMBALI WAKUTANA KWENYE SEMINA NA KONGAMANO JIJINI ARUSHA


Mch.Dr.Jerry Williamson kutoka nchi Marekani akiomba katika ibada ya katika kongamano kanisa la  Zion lililopo Njiro jijini Arusha ambapo kanisa hilo limeendaa semina na
kongamano kwa wachungaji pamoja na washirika wengine,kulia kwake ni  Ben Mangeni ambaye ni mkalimani wake
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kongamano hilo
Mch.George Mngodo akiongea na waandishi wa habari alisema kuwa watu ambao wataweza kushiriki kongamano hilo wataweza kujifunza mambo ambayo awali hawakuweza kuyafahamu ambayo yatawawezesha kuvuka kutoka hatua moja kwenda nyingine
Mmoja wa wachungaji wa kanisa hilo Paul Sulley akiongea na waandishi wa habari  ambapo alisema matarajio yao ni kuona kila mtumishianayehudhuria anavuviwa upya ili aweze kumtumikia Mungu kwa bidii.
Kushoto ni Mtume Trice Shumbusho akiwa na mkalimani wake akihubiri katika kongamano hilo
Waumini wakiwa katika maombi
Baadhi ya wageni wakiwa katika kanisa la Zion kwa ajili ya kongamano
Baadhi ya wageni wakiwa katika kanisa la Zion kwa ajili ya kongamano
Picha ikionyesha madhabahuni
Picha ikionyesha jengo la kanisa

******
Wachungaji zaidi ya 300 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini bila kujali madhehebu yao wako katika semina maalumu ya neno la Mungu yenye lengo la kusaidia kupeleka ujumbe wa madhihilisho ya nguvu ya kristo katika maeneo mbalimbali ya nchi ili watu waweze kubadilika na kumjua Mungu.

Semina hiyo ya siku nane iliyoandaliwa na kanisa la Zion City Church Arusha itafanyika kanisani hapo ikiambatana na Kongamano ambalo limeandaliwa kwa ajili ya wachungaji na
watu mbalimbali likiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa kupeleka injili kwa watu
wa mataifa.


Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kongamano hilo Mch.George Mngodo alisema kuwa watu ambao wataweza
kushiriki wataweza kujifunza mambo ambayo awali hawakuweza kuyafahamu ambayo yatawawezesha kuvuka kutoka hatua moja
kwenda nyingine.


Mngodo aliongeza kuwa huduma zitakazo tolewa katika katika
kongamano hilo hazitawakugusa kiroho tu bali hata kwenye maisha yao ya kawaida
wataweza kubadilika 

“Tunaamini kongamnao hili litagusa wachungaji hawa na jamii wanayoihudumia kimwili na kiroho”alisema Mngodo

Kwa upande wake mmoja wa wachungaji wa kanisa hilo Paul Sulley alisema kuwa matarajio yao ni kuona kila mtumishi anayehudhuria anavuviwa upya ili aweze kumtumikia Mungu kwa bidii.

Mch.Sule alisema kuwa ulimwengu wa sasa umeharibika hivyo unahitaji watumishi waliokutana na Mungu na si wanaomjua Mungu pekee ili waweze kuwatumikia watu.

Miongoni mwa watumishi wa Mungu wa kimataifa watakao kuwa wasemaji wakuu katika kongamano hilo ni Askofumkuu wa kanisa la Zion City Church Arusha John Shumbusho pamoja na mkewe Trice Shumbusho 

Wachungaji wengine ni kutoka nje ya nchi Mch.Dr.Jerry
Williamson, Mch.Dr Jim Oxendine kutoka Marekani,Mch.Yoshua Masasu kutoka Rwanda,Mch.Aloysius Kiiza kutoka Uganda,Pamoja na Mch.George Mkandawire kutoka Afrika
Kusini.
Na Pamela Mollel,Arusha

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com