SERIKALI YAAGIZA MAKAMPUNI YA UCHIMBAJI MADINI KUTOA ELIMU YA USALAMA KWA WACHIMBAJI WADOGO,WAZIRI MHAGAMA ATEMBELEA MABANDA YA ACACIA



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama ameiagiza migodi mikubwa nchini Tanzania kuanzisha programu maalum kwa ajili ya kutoa elimu ya afya na usalama kwa wachimbaji wadogo wa madini ili kuepuka ajali zinazotokea kwenye maeneo ya migodi.


Waziri Mhagama ametoa agizo hilo leo Ijumaa Aprili 28,2017 katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro wakati akikagua mabanda ya maonesho ya migodi mbalimbali nchini ikiwemo inayomilikiwa na kampuni ya Acacia inayomiliki migodi ya Bulyanhulu,Buzwagi na North Mara.

“Serikali imeridhishwa kuhusu namna migodi mikubwa nchini inavyozingatia suala la usalama na afya mahali pa kazi,migodi hii mikubwa inatakiwa kutengeneza program maalumu za kufundisha migodi midogo midogo inayowazunguka ili watanzania wote waweze kujua namna gani wanaweza kuwa salama katika shughuli za uchimbaji madini”,alisema Mhagama.

“Tumekubaliana mwaka ujao kila mgodi utatoa taarifa namna gani kuwasaidia watanzania kuwa salama katika maeneo ya kazi”,alieleza Mhagama.

Akizungumza katika mabanda ya Kampuni ya uchimbaji madini ya  dhahabu ya Acacia inayomiliki migodi ya Buzwagi,Bulyanhulu na North Mara,Mhagama alieleza kufurahishwa kuhusu namna kampuni hiyo inavyokusanya na kutumia takwimu za afya na usalama mgodini.

Waziri Mhagama alikuwa mgeni rasmi katika siku ya Usalama na afya mahali pa kazi duniani kitaifa mkoani Kilimanjaro.

Nimekuwekea hapa picha za matukio wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akitembelea mabanda ya kampuni ya Uchimbaji madini ya Acacia
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akiwa katika banda la mgodi wa Bulyanhulu katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi kwa ajili ya kuangalia vifaa vya kisasa vinavyotumika katika uokoaji na namna mgodi huo unavyofanya katika kuhakikisha wafanyakazi wao wanakuwa salama mgodini
Kulia ni Afisa Uhakiki wa Usalama mgodi wa Bulyanhulu Amina Mohamed akimweleza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama kuhusu namna wanavyokusanya takwimu za afya na usalama mgodini
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akiangalia vifaa vya kisasa vinavyotumika katika kutunza takwimu za afya na usalama katika mgodi wa Bulyanhulu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akisisitiza maafisa kutoka mgodi wa Bulyanhulu kuanzisha programu maalumu ya utoaji elimu ya usalama na afya kwa  wachimbaji wadogo wadogo wa madini
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akizungumza na maafisa kutoka mgodi wa Bulyanhulu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akiangalia kitabu maalumu kinachotumika kukusanya takwimu za afya na usalama katika mgodi wa Bulyanhulu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akizungumza jambo na Kiongozi wa kitengo cha afya mgodi wa Bulyanhulu Dkt. Kudra Said (kushoto).Katikati ni Afisa Mahusiano mgodi  wa Bulyanhulu Mary Lupamba
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akifurahia jambo na maafisa kutoka mgodi wa Bulyanhulu
Kulia ni Kiongozi wa Idara ya Mahusiano ya Jamii mgodi wa North Mara Fatuma Mssumi akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama katika banda la mgodi wa North Mara
Afisa Usalama na Afya mgodi wa North Mara Alfred Mwema akielezea kuhusu namna mgodi huo unavyozingatia masuala ya usalama mgodini.Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akizungumza katika banda la mgodi wa Bulyanhulu
Kulia ni Dkt. Ludovick Silima kutoka mgodi wa Buzwagi akionesha vifaa vya uokoaji vinavyotumiwa na mgodi huo wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama alipotembelea banda la mgodi wa Buzwagi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akizungumza katika banda la mgodi wa Buzwagi. Aliyeshikilia kipaza sauti ni Kaimu Mtendaji kutoka OSHA Hadija Mwenda
Kulia ni Mkufunzi Idara ya Uokoaji Mgodi wa Buzwagi Azael Kitange akionesha takwimu za afya na usalama za mgodi huo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akisikiliza kwa umakini maelezo kutoka kwa Mkufunzi Idara ya Uokoaji Mgodi wa Buzwagi Azael Kitange.Kushoto ni Afisa Mawasiliano mgodi wa Buzwagi Magesa Magesa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akiondoka katika mabanda ya kampuni ya Acacia inayomiliki migodi ya North Mara,Buzwagi na Bulyanhulu.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post