Msanii Afande Sele amefunguka mengine mapya kwa kudai shindano la Miss Tanzania kwa sasa linatia aibu kubwa katika taifa kwa kukosa hadhi huku likionekana ni shindano linalomnufainisha mtu mmoja nasiyo taifa kama ilivyokuwa awali.
Afande Sele amesema hayo baada ya watu wengi ndani na nje ya nchi kutoridhishwa na zawadi ya gari aliyopewa Miss Tanzania 2016/2017, Diana Edward wakidai limechakaa na linashusha hadhi ya mashindano hayo pamoja na kuvunja moyo watu ambao walikuwa na lengo la kushiriki katika mashindano mengine yajayo.
“Utapeli ni nini ?....Gari ya Miss Tanzania 2017 na gari ya Miss Tanzania 2011 zinatoa jibu la swali hilo…Lakini pia ni vyema tukamuomba waziri husika katika masuala hayo …a.k.a Dk. Marufuku akamuulize muandaaji wa Miss Tanzania kama ni kweli ameaumua kuzeeka labda hata kufa na shindano lake?”. Ameandika Afande Sele kupitia mtandao wake wa kijamii Instagram
Msanii huyo aliendelea kwa kusema “Kama kweli iko hivyo basi itoshe pia kubadili jina la shindano kwa kuliita Miss jina lake badala ya kuendelea kutia aibu Taifa kwa kuliita Miss Tanzania huku likikosa hadhi ya kitaifa katika maeneo yote kwa makusudi na maslahi yake yeye mtu mmoja tu…aibu yake aibu yetu…Imetosha sasa…imetosha sana”.
Social Plugin