Sinu ya Essential hutumia mfumo wa Android na imeanza kuuzwa nchini Marekani kwa dola $699.
Andy Rubin, ambaye ni miongoni mwa watu waliobuni programu ya software Android ya Google, amezindua simu yake ya smartphone yenye ncha ndefu.
Bwana Rubin aliacha kazi katika Google mwaka 2014 kwa ajili ya kubuni kampuni yake ya uwekezaji wa kiteknolojia.
Essential ni moja wapo ya kampuni zinazodhaminiwa na kampuni ya Rubin - na simu ya Essential ni moja bidhaa zake.
Simu hiyo hutumia mfumo wa Android na imeanza kuuzwa nchini Marekani kwa dola $699.
Hata hivyo, itakuwa ni vigumu kwa kampuni hiyo kujipenyeza katika masoko makubwa ya ambayo tayari yameimarisha mauzo ya bidhaa zake nchini humo.
Samsung kwa sasa ndio yenye soko kubwa la hisa katika soko la simu za Smart, ikiwa na mauzo ya asilimia 21% kote duniani, kulingana na mchambuzi wa masuala ya makampuni Gartner. Apple ina soko la asilimia 14%.Kioo cha simu ya Essential kimefunika karibu uso wote wa simu
Licha ya makampuni makubwa ya Uchina yanayouza simu zenye gharama ya chini, viwanda vidogo vidogo vimepata ugumu wa kupata walau asilimia moja ya hisa kwenye soko za bidhaa zao - na bei ya simu ya Essential inaiweka kwenye hali ya changamoto kubwa zaidi
Lakini Bwana Rubin aliiambia hadhira ya watu mjini California kwamba anaamini kuna nafasi ya soko la Android kwa muuzaji mwingine licha ya Samsung, na kwamba Essential inalenga kuwa kampuni kuu inayotoa aina mbali mbali za bidhaa kwa mnunuzi
Essential phone imetengenezwa kwa madini ya titanium na ina kioo kilichoenea sehemu kubwa ya simu na sehemu isiyo na kioo ni ndogo zaidi.
Via>>BBC
Social Plugin