UNGUJA: Polisi mmoja kwa jina Abbasi Anali amefariki dunia kutokana na kusombwa na maji huko Unguja, Zanzibar.
Taarifa zilizotufikia zinaonesha kwamba askari huyo ambaye alikuwa mpiga picha wa Polisi, alikuwa akiendesha pikipiki maarufu kama Vespa, kutoka mjini Unguja kuelekea Makunduchi.
Mwandishi wa habari Bi Jazaa aliyefika katika eneo la tukio hilo anasema, “Ajali hiyo imetokea leo hii Ijumaa tarehe 12 Mei, 2017…na ilikuwa baina ya saa 5 na 6 hivi.” Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Nassir, amethibitisha kifo cha askari huyo, na kuongeza kwamba tayari mwili wake umepatikana.
Uchunguzi wa mwili huo unaendelea katika Hospitali ya Mnazi Mmoja. “Mauti yamemfika alipojaribu kuvuka katika eneo la Kibonde mzungu, Fuoni ambapo kulikuwa na maji mengi,” Jazaa.
Watu walioshuhudia tukio hilo wanasema eneo hilo lliikuwa limetapakaa maji kutokana na mvua kunyesha na kuziba barabara kuu. wanasema asakari huyo amekosa mwelekeo wakati anavuka na kutumbukia kwenye maji mengi.
Mvua kubwa inayoendelea kunyesha hasa kwenye maeneo ya ukanda wa Pwani, imesababisha madhara mengi ikiwa ni pamoja na vifo katika baadhi ya maeneo, nyumba kuanguka, magari kukwama au kuharibika, na miundombinu mingi kuharibika, hususan barabara.
Mamlaka ya Hali ya Kewa Tanzania imetoa taarifa inayoonesha ukanda wa Pwani unaendelea kupata mvua za kiasi cha 50mm ndani ya kipindi cha saa 24. Na kwakesho tarehe 13 May, 2017, “kuna Angalizo la Matarajio ya kuwepo Vipindi vifupi vya Mvua kubwa,” Kwa mujibu wa taarifa za tovuti yao.
Kwa upande wa Zanzibar, maeneo yaliyoharibika zaidi ni pamoja na Mwanakwerekwe, Kibonde mzungu, Ziwa maboga, Mtoni kidato, Jeng’ombe, na Sebleni kwa wazee.
Chanzo-http://tanzanianzima.com
Social Plugin