Mwanamuziki,Diamond Plantinumz alikuwa nchini Kenya kwa ajili ya tamasha la Koroga ambalo lilifanyika jana Jumapili Mei 28,2017
Diamond aliwahutubia wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi na kuzungumzia kifo cha aliyekuwa mme wa mkewe wa sasa, Ivan Ssemwanga
Ssemwanga alifariki akiwa amelazwa katika hospitali moja nchini Afrika Kusini baada ya kukumbwa na mshtuko wa moyo
****
Mwanamuziki, Diamond Plantinumz amezungumzia kifo cha aliyekuwa mme wa mkewe ,Zari Hassan ambaye alifariki juma lililopita akipokea matibabu katika hospitali moja Afrika kusini.
Akizungumza akiwa katika chuo kikuu cha Nairobi Ijumaa Mei 26, Diamond alisema kuwa Zari anapitia wakati mgumu ikizingatiwa kuwa alizaa watoto watatu na Ssemwanga .
Aidha ,Diamond alisema kuwa hangekosa kwenda Kenya kuhudhuria tamasha la Koroga kwa sababu alikuwa tayari amewaahidi Wakenya kwamba angeenda kabla ya msiba huo kutokea.
Diamond alisema atahudhuria mazishi ya mwenzake,Ssemwanga.
"Kwa kweli umekuwa ni wakati mgumu kufutilia mbali mualiko huu. Nimeongea na mke wangu akanielewa. Nikimaliza hapa nitaenda Uganda kwa sababu ya mazishi," Diamond alisema.
Marehemu Ivan Ssemwanga alikuwa amemuoa Zari Hassan ambaye kwa pamoja walikuwa na watoto watatu wa kiume kabla ya kutalakiana kisha Zari akaolewa na Diamond.
Social Plugin