Wasanii wa kizazi kipya Fid Q, Snura, Madee, Dogo Janja, Stamina na Navy Kenzo wanatarajia kutoa burundani katika matamasha ya Taifa Moja ambayo yatafanyika kesho (Jumamosi) kwenye mikoa minne tofauti hapa nchini.
Burandani hiyo itaenda sambamba na kutoa elimu kwa Wananchi wa mikoa husika juu ya uhuru wa kutuma pesa bila mipaka ambayo ni ushirikiano wa makampuni matatu ya simu za mkononi kupitiia huduma zao Tigo Pesa, Airtel Money na Ezy Pesa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Liginiku Milinga ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Fern Tanzania ambao ndio waratibu na waandaaji wa matamasha hayo alisema wasanii wote washathibitisha kushiriki kwao kwenye matamasha hayo na kwamba maandalizi yote yamekamilika huku akiwaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kupata burundani toka kwa wasanii wakali hapa nchini na pia kupata elimu juu ya kutuma na kupokea pesa kwenda mtandao wowote hapa Tanzania kwa gharama ile ile.
Wasanii Stamina na Fid Q watambuiza kwenye tamasha litakalofanyika kwenye uwanja wa Mwembetongwa mjini Iringa wakati Dogo janja na Baba Levo wakifanya ya kwao kwenye uwanja wa Community Center grounds uliopo mjini Kigoma huku Snura na Madee wakiwashika vilivyo wakazi wa mji wa Tanga kwenye uwanja wa Tangamano. Navy Kenzo huku akitamba na wimbo wake wa kamati ya chini, atakuwa kwenye uwanja wa shule ya msingi ya Sabasaba iliyopo mjini Morogoro.
Tangu tuanze kampeni yetu ya Taifa Moja tumekuwa tukitumia wasanii wetu kutoa elimu kwe Wananchi kupitia burudani na tumetapata mafanikio makubwa sana ya kufikisha ujumbe wetu wa uhuru wa kutuma pesa bila mipaka kupitia burudani kwa Watanzani. Naomba nitoe wito wangu kuwaomba Watanzania wajitokeze kwa wingi kesho kushuhudia wasanii wetu ambao wamehaidi kutoa burundani ya uhakika.
Bali na kupata burundani, Watanzania wataweza kufahamu jinsi ya kujikwamua kiuchumi kwani kwa njia ya kutuma pesa kwenda mtandao wowote ule kwa gharama ile ile imetoa urahisi kwa kuongeza watumiaji wengi wa huduma ya kutuma pesa na hivyo kuwa rahisi Wananchi kupata huduma za kifedha.
Taifa Moja ni kampeini ambayo imedhaminiwa na taasisi za Financial Sector Deepening Trust of Tanzania (FSDT) pamoja na Bill & Melinda Gates Foundation huku ikiratibiwa na International Finance Corporation (IFC) chini ya muungano ya makampuni matatu ya simu za mkononi za Airtel Tanzania, Tigo Tanzania na Zantel kupitia huduma zao za Airtel Money, Tigo Pesa na Ezy Pesa.
Social Plugin