FUNDI ujenzi wa ghorofa la MNF Square lililoko katikati ya jiji la Dar es Salaam, amefariki dunia papo hapo baada ya kuteleza kutoka ghorofa ya 16.
Watu walioshudia tukio hilo wamesema kuwa fundi huyo alianguka juzi saa 10:00 alasiri katika ghorofa hilo wakati wakiendelea na kazi ya ujenzi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salumu Hamduni, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Social Plugin