Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba SC, Haji Manara amedai anaonewa kwa kupewa lawama zisizomuhusu baada ya kile kinachoaminiwa kuwa naye ni miongoni mwa viongozi walioshiriki katika makubaliano na mdhamini wao mpya Sportpesa
Manara amesema hayo siku moja baada ya mfanyabiashara , Mohammed Dewji kutoa kauli ya kusikitishwa na uongozi wa klabu ya Simba kusaini mkataba wa udhamini wa muda mrefu na Sportpesa bila ya kumshirikisha yeye, ambaye aliweka nguvu zake nyingi katika klabu hiyo.
“Uongozi wowote ni Jalala ila uongozi wa mpira ni Dampo, ‘sometimes’ napokea lawama zisizonihusu, ‘but’ nina moyo wa chuma na nina uzoefu wa kuwa kiongozi katika tasnia tofauti, kazi yangu ni kuhabarisha umma, mengine ni kunionea”ameandika Manara kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Aidha, Manara amesema kuwa hakuhusika kwa chochote katika mchakato huo lakini kwakuwa yeye nikiongozi amesema yuko tayari kupokea lawama zote zinazoelekezwa kwake na baadhi ya wanachama.
Social Plugin