Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hanspope amerudi kundini Simba baada ya kufuta uamuzi wake wa kujiuzulu
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara amethibitisha suala hilo na kusema Hanspope amerudi kundini baada ya kujiuzulu kutokana na sakata liloendelea ndani ya Simba.
"Rasmi Hanspope arejea kundini, afuta uamuzi wake wa kujiuzulu na ndio maana 'fans' wetu nawaomba mtulie hakuna kitakachoharibika, ni upepo mbaya ulipita na sasa umetulia, karibu tena kamanda Pope" alisema Haji Manara
Social Plugin