Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HAWA NDIYO WANYAMA SITA WALIOWAHI KUGOMBEA NAFASI ZA JUU ZAIDI ZA UONGOZI DUNIANI

Kwa kawaida uongozi ni dhamana kubwa wanayopewa Watu mbalimbali lakini hii ya Wanyama inaweza kukuacha hoi kidogo….. kwenye nchi za wenzetu Jamii huamua kumsimamisha Mnyama kugombea nafasi flani ya uongozi kama njia ya kuonesha kuchoka kuchagua viongozi ambao hawatimizi ahadi zao.

Leo nimekutana na hii stori kuhusu wanyama sita waliowahi kugombea na wengine kushinda  nafasi za juu za uongozi katika nchi mbalimbali duniani.
1:Moris
Huyu ni paka ambaye aligombea nafasi ya Umeya katika mji wa Xalapa Mexico mwaka 2013 ambapo hakushinda lakini aliweza kumtoa jasho mpinzani wake Julio Hernández ambaye alikiri kuogopa kuangushwa na Paka huyo kwenye nafasi yake kwani umaarufu aliokuwa nao Moriss haukuwa wa kawaida.
2: Duke
Unaweza usiamini lakini Meya wa Minnesota Marekani ni Mbwa na alishinda umeya August 2016 ikiwa ni mara ya tatu kushinda kuwa meya wa jimbo hilo kama ilivyo kwa wagombea wengine Duke alipata wadhamini ambao kila mmoja alilipa dola milioni moja ili kudhamini harakati zake za kisiasa.
           Hapa Duke alikuwa akihojiwa na waandishi wa habari kuelezea ushindi wake
3: Cacareco  
Cacareco ni Faru ambaye alishinda Ubunge katika mji wa Sao Paolo Brazil mwaka 1959, Wananchi wa eneo hilo waliamua kumchagua Faru kama kiongozi wao baada ya kuchoka Wanasiasa waongo ambao hawatimizi ahadi zao ambapo baada ya Cacareco kushinda uchaguzi ulirudiwa na akachuguliwa Binadamu.
4:Pigasus
Mwaka 1968 chama cha Youth International kilimchagua Nguruwe kuwa mgombea wao wa kiti cha Urais MarekaniPigasus hakuweza kuendelea kuwakilisha chama hicho baada ya manispaa kukataza kuleta wanyama maeneo ya mijini lakini aliendelea kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa miaka 3.
 Hapa Pigasus alikuwa akitambulishwa kwa wapiga kura wake Chicago, Marekani
5:Macaco Tiao
Huyu ni Nyani ambaye aligombea nafasi ya umeya katika jiji la Rio de Janeiro Brazil mwaka 1988 na kupata kura 400,000 na kuweza kushika nafasi ya 3 kati ya wagombea 12.
6: Yasha 
Yasha ni Kasuku aliyegombea nafasi ya udiwani katika mji wa Belarus, Urusi mwaka 2014 lakini aliamua kujiengua katika kinyanganyiro hicho kwasababu alipenda agombee nafasi kubwa zaidi ya uongozi na unaambiwa alikuwa anaweza kuongea maneno kama “Pesa ziko wapi” na “ninataka kwenda kwenye baraza la madiwani”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com