Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HII HAPA ORODHA YA NCHI ZENYE WATU WANENE ZAIDI DUNIANI

Mtandao wa CIA’S World Fact umetoa orodha ya nchi zenye idadi kubwa ya watu wanene duniani ambapo Amerika ya Kaskazini ikiwa na nchi nyingi zenye idadi kubwa huku Qatar na Kuwait zikiongoza Bara la Asia na Afrika kukiwa na idadi ndogo ya watu wanene.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo zaidi ya 75% ya watu katika nchi hizi wana uzito uliopitiliza huku wanawake wakiongoza kwa unene ukilinganisha na wanaume katika nchi za kiarabu wakati Canada, Marekani na Australia wanaume wanaongoza kwa zaidi ya 25% dhidi ya wanawake.

Shirika la Afya Duniani ‘WHO’ limesema sababu za nchi hizi kuwa na idadi kubwa ya watu wanene hazihusiani na Uchumi mkubwa katika nchi hizo bali upatikanaji wa vyakula visivyokuwa na virutubisho ambavyo wanakula hasa kutoka viwandani ukilinganisha na nchi za Afrika.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com