Huu ni ulimwengu wa kanuni, taratibu na sheria ambazo kufuatwa ni wajibu wa kila mtu ingawa zipo kanuni, taratibu na sheria nyingine zinaajabisha sana na ninazo hapa sheria 8 kwenye sehemu mbalimbali za dunia.
1: Polisi kukamata wenye UKIMWI – Ugiriki
Nchini Ugiriki Polisi wanaruhusiwa kumkamata Mtu yeyote anayeshukiwa kuwa na HIV… Polisi pia wanaruhusiwa kulazimisha watu kupima HIV, kutangaza majina ya wenye HIV hadharani na kuwafungia majumbani mwao.
2: Ruhusa ya kumpiga mkeo – Arkansas
Katika mji wa Arkansas, Marekani bado kuna sheria ambayo ilianzishwa miaka ya 1800 ambayo inamruhusu mume kumpiga mkewe lakini mara moja kwa mwezi.
3: Mwenye mustachi haruhusiwi kubusu – Iowa
Kuwa na mustachi au hata ndevu sio tatizo katika sehemu nyingi duniani lakini katika mji wa Iowa Marekani ni kama vile unaambiwa usiwe na mustachi kiaina baada ya watu wenye mustachi kukatazwa kumbusu mwanamke hadharani.
4: Tangazo la ndoa kwenye gazeti – Ugiriki
Nchini Ugiriki kama unataka kuoa, sheria inawataka wenye nia ya kufanya hivyo kuchapisha tangazo la ndoa kwenye gazeti (kwa kigiriki) au kwenye ubao wa matangazo.
5: Mke kumuua Mumewe msaliti – Hong Kong
Hong Kong kuna sheria ambayo inaruhusu Mke kumuua Mumewe kama atabaini anamsaliti ambapo hata hivyo anatakiwa kumuua kwa mikono yake pasipo kutumia silaha yoyote.
6: Kusahau Birthday ya mkeo – Samoa
Ni wangapi huwa na kumbukumbu nzuri ya siku ambayo wamezaliwa watu wao wa karibu hasa Mke/Mume? Unaambiwa kwenye nchi ya Samoa ni kosa kwa mume kusahau birthday ya mkewe.
7: Matembezi na Mbwa – Turin, Italia
Baadhi ya sehemu ni jambo lisilo la kawaida mtu kutembea na mbwa katika matembezi ya kawaida lakini hilo ni tofauti katika mji wa Turin, Italia ambapo wamiliki wa Mbwa wanatakiwa kutembea na Mbwa wao angalau mara tatu kwa siku.
8: Kuibia mitihani – Bangladeshi
Hakuna nchi inayoruhusu Wanafunzi wake waibie majibu wakati wa mitihani, unaambiwa Bangladeshi imeweka sheria kuwa watoto wa miaka 15 na watu wazima, wanaweza kufungwa kama watakutwa na kosa la kuibia kwenye mitihani yao ya mwisho.
Social Plugin