Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HOUSE GIRL AJIUA KWA KUJICHOMA KISU DAR

Katika hali isiyo ya kawaida dada wa kazi aliyetambulika kwa jina la Christina Mabuga (37), amekutwa ameuawa ndani ya chumba chake, huko Moshi Baa, Gongo la Mboto, Dar es Salaam kwa kujichoma kisu kifuani.


Jeshi la Polisi katika mkoa wa kipolisi Ilala limethibitisha kutokea kwa tukio hilo, lililofanyika katika nyumba ya mwajiri wa dada huyo wa kazi, ambapo mpaka sasa haijafamika chanzo cha dada huyo kujiua.

Mwajiri wa binti huyo, Anna Kasanda alisema alipokea taarifa saa 9:00 alasiri kwamba kuna tatizo nyumbani kwake, na ndipo alipoamua kurudi nyumbani na kukuta mfanyakazi huyo amejiua.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Chanzo-Blog ya wananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com