Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema) Godbless Lema ameuliza swali je, Yeriko Nyerere amekamatwa au ametekwa?
Lema ameuliza swali hilo katika ukurasa wake wa Twitter leo na kuongeza: “Msiogope. Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea. "
Yeriko anayefahamika kuwa ni kada wa Chadema, amekamatwa leo saa tisa alfajiri na watu wanaodhaniwa kuwa ni polisi akiwa nyumbani kwake, Kigamboni, Mbutu.
Meya wa Ubungo, Boniphace Jacob amethibitisha kukamatwa kwa Yeriko.
Yerico amekamatwa au ametekwa ? MSIOGOPE. Kwani imeandikwa "Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea "— Godbless E.J. Lema (@godbless_lema) May 31, 2017
Kada wa Chadema Yeriko Nyerere, amekamatwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni polisi akiwa nyumbani kwake Kigamboni, Mbutu.
Taarifa iliyotolewa na Meya wa Ubungo, Boniphace Jacob imeeleza kuwa Nyerere alikamatwa na watu hao ambao waliambatana na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbutu.
“Nimepata taarifa kutoka kwa ndugu wa Yeriko ambao wamenipigia simu alfajiri leo. Wamesema amekamatwa saa tisa usiku na watu hao ambao walivalia kiraia. Viongozi wa Chadema wanaelekea polisi kufuatilia kwa kina chanzo cha Yeriko kukamatwa,” amesema Jacob
Social Plugin