Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela amewataka wadau wa sekta ya afya mkoani Shinyanga kufanya kazi kwa ushirikiano,umoja na uwazi ili kuhakikisha changamoto zilizopo katika sekta hiyo zinapungua kwa ajili ya maendeleo ya jamii.
Msovela ametoa rai hiyo leo wakati wa kufunga kikao siku mbili cha wadau wa sekta ya afya mkoa wa Shinyanga kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa kuanzia May 30,2017 hadi May 31,2017 kilichokutanisha pamoja mashirika na taasisi zaidi ya 30 zinazojishughulisha na masuala ya afya.
Msovela alisema serikali mkoa wa Shinyanga inatambua kazi nzuri zinazofanywa na mashirika na taasisi katika kushughulikia masuala ya afya hivyo kuwataka waungane pamoja badala ya kila mmoja kufanya kazi peke yake ili kumaliza changamoto zinazoikabili sekta hiyo.
Aidha Msovela alitoa wito kwa wadau wote wa afya wanapoanza kutekeleza miradi mipya waripoti katika ngazi ya mkoa na wilaya huku akiwasisitiza kuwasilisha mipango kazi yao sambamba na kuwa wa wazi ili kuepuka migongano inayoweza kujitokeza.
ANGALIA HAPA PICHA ZA MATUKIO
Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akizungumza wakati wa kufunga kikao cha wadau wa afya mkoa wa Shinyanga
Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akizungumzia kuhusu umuhimu wa wadau wa afya kukutana na kujadili masuala ya afya katika jamii
Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akizungumza na wadau wa sekta ya afya mkoa wa Shinyanga
Mtaalamu wa magonjwa ya mlipuko,Athanas Lucas akielezea kuhusu magonjwa ya mlipuko ambapo aliitaka jamii kuchukua tahadhali juu ya magonjwa ya mlipukovile Ebola,Surua na Rubella,polio,pepopunda ya watoto wachanga,kipindupindu,homa ya uti wa mgongo na kichaa cha mbwa.
Kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela na Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Dkt. Rashid Mfaume wakisikiliza kwa makini mada kuhusu magonjwa ya mlipuko
Mtaalamu wa magonjwa ya mlipuko,Athanas Lucas akiendelea kutoa mada kuhusu magonjwa ya mlipuko
Mkurugenzi wa Shirika la AGAPE,John Myola akielezea kuhusu shughuli zinazofanywa na shirika hilo katika kupiga vita vitendo vya ndoa na mimba za utotoni
Wajumbe wa kikao hicho wakiwa ukumbini
Mratibu wa damu salama mkoa wa Shinyanga,Joel David akielezea kuhusu mahitaji ya damu mkoa wa Shinyanga ambapo aliomba wadau waendelee kujitokeza kutoa damu ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa damu katika hospitali mbalimbali mkoani Shinyanga
Mdau wa afya,Mzee Sengerema akichangia hoja wakati wa kikao hicho
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Dkt. Rashid Mfaume akizungumza wakati wa kikao hicho ambapo aliwashukuru wadau wa sekta ya afya kujitokeza kwa wingi kujadili masuala yanayohusu afya mkoani humo.Angalia Picha Nyingi zaidi <<HAPA>>
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Social Plugin