Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema na aliyekuwa Waziri Mkuu, Mh. Edward Lowassa amelaani vikali kitendo cha serikali ya Mkoa wa Dar es salam kuzuia kongamano la demokrasia lililopangwa kufanyika siku ya jana may 13, Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Mhe. Lowassa jana akizungumza na wanahabari ofisini kwake Mikocheni, Dar alisema kuwa amesikitishwa sana na serikali kuzuia kongamano ambalo lilikuwa na nia njema ya kuzungumza kuhusu demokrasia na kujifunza kutoka kwa watu mbali mbali jinsi ya kufanya siasa bila kukosea na kurekebishana penye makosa.
Mjumbe huyo aliendelea kufafanua kwamba hakuna tatizo kwa vyama vya siasa kutofautiana mawazo kwani ndiyo demokrasia na ndiyo sababu kubwa ya waandaji kushirikisha watu wenye taaluma tofauti tofauti katika kongamano hilo.
"Chadema kwa ujumla tunalaani sana kitendo cha Serikali ya Dar es salaam kuzuia mkutano wa amani wa kuwaunganisha watanzania pamoja kwa kutumia kongamano la demokrasia.
"Kitendo ambacho kimefanywa ni kuminya demokrasia. Nia ilikuwa njema na ndio maana waandaji wa kongamano waliweka picha yangu na kinana tukiwa tunatabasamu hivyo hakuna dhambi kwenye kutofautiana mawazo"- alisema Lowassa.
Taarifa iliyotolewa jana kuhusu kongamano.
Hata hivyo Mhe. Lowassa amekitaka chama cha Mapinduzi kutonyayasa upinzani kwa kuwa hawataweza kukaa madarakani muda wote huku akiwatahadharisha wakumbuke vyama vya ukombozi wa Afrika vilivyobaki madarakani ni ANC na CCM.
Social Plugin