Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU KUONGOZA WAOMBOLEZAJI VIFO VYA WANAFUNZI ARUSHA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan aliwasili mjini Arusha jana jioni ambapo leo ataongoza wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa ya jirani katika kuaga miili ya wanafunzi 32,walimu wawili pamoja na dereva mmoja wa shule ya Lucky Vicent iliyopo Jijini Arusha waliopata ajali juzi tarehe 06-May-2017 katika eneo la Rhotia wilayani Karatu mkoani Arusha.


Wanafunzi na walimu hao walipata ajali hiyo wakati wanaenda kwenye shule iitwayo Tumaini kwa ajili ya kufanya mitihani wa ujirani mwema baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kutumbukia korongoni kwenye eneo la Rhotia wilayani Karatu.


Ibada na dua za kuaga miili ya marehemu hao itafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha kuanzia Saa Mbili asubuhi hii

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com