Mchango wa Mbunge wa Kuteuliwa(CCM), Salma Kikwete kuhusu kupinga wanafunzi wanaopata mimba wakiwa shuleni kuruhusiwa kuendelea na masomo jana ulizua gumzo bungeni kutokana na wabunge kugawanywa na suala hilo.
Hali hiyo ilijitokeza wakati wabunge waliokuwa wakichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa Fedha 2017/18 bungeni jana.
Salma amesema anapinga suala la watoto wanaopata ujauzito shuleni kuendelea na masomo kutokana na mila, desturi, dini na mazingira.
Ameitaka Serikali kutafuta njia nyingine ya watoto hao kupata elimu badala ya kuwaruhusu kuendelea na masomo.
Akitoa taarifa yake kwa mchangiaji Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy alitaka mbunge yeyote ndani ya Bunge ambaye alianza kushiriki mapenzi akiwa shuleni atoe ushuhuda bungeni kama aliweza kuendelea vizuri kimasomo.
Amesema anaunga mkono wanafunzi wanaopata mimba wakiwa shuleni wasiruhusiwe kuendelea na masomo
Social Plugin