Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MASOUD KIPANYA: HAKUNA MWANAMME ANAYEPENDA MWANAMKE MMOJA...TUNAJIZUIA TU KWA SABABU


Mtangazaji na Mchoraji katuni maarufu nchini Tanzania,Masoud Kipanya amewaaacha watanzania midomo wazi kwa kuweka wazi maoni yake kuwa mwanaume hawezi kuridhika na mwanamke mmoja.

Masoud amesema tangu zamani wanaume ni Watu mwenye tamaa hivyo hakuna mwanaume ambae anapenda kuwa na mwanamke mmoja ila ni vitu vidogo vidogo tu vinavyozuia kama dini ya Kikristo na masuala mengine ya kiuchumi.

“Hakuna mwanaume anaependa kuwa na mwanamke mmoja,na hiyo ndiyo huruka ya uanaume,tunajizuia tu kwa sababu!! hivyo kwa mfano kwa wenzangu wakristo utaratibu unawazuia lakini angalia vidumu vilivyo nje unaona eeehh??“Amesema Masoud Kipanya kwenye Mahojiano yake na Kwanza TV.

Hata hivyo Masoud alizungumzia suala la idadi ya kuzaa watoto kwenye familia na kusema kuwa kwa upande wake  yeye hana kikomo kwenye kuzaa kwani anaamini watoto hawalishwi na yeye bali wanalishwa na mwenyezi Mungu.

Masoud Kipanya kwa mujibu wa Takwimu za mwaka jana zilizofanywa na kituo cha Clouds FM kupitia kipindi cha XXl ni moja ya watu watatu maarufu nchini Tanzania wanaoendesha magari ya kifahari akiwa anamiliki gari aina ya Hummer H3.

==>Msikilize hapo chini akiongea

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com