Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) amekabidhi msaada wa vifaa tiba katika vituo vya afya na zanahati zilizopo wilaya ya Shinyanga na Kishapu ili kukabiliana na vifo vya mama na mtoto vinavyotokana na uzazi.
Vifaa hivyo ni vitanda 15 vya kisasa vya kujifungulia akina mama wajawazito ,vifaa vinavyotumika katika chumba cha kujifungulia (delivery kit 1) ,vitanda 15 vya kulalia wagonjwa,magodoro 15,mashuka 30,viti 15 vya wagonjwa vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 33.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo kwa nyakati mbalimbali wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo,Hamad alisema vifaa hivyo vimetolewa na ubalozi wa China nchini Tanzania.
“Mimi ni mama nafahamu vyema matatizo yanayowakabili akina mama,hali hiyo ndiyo iliyonifanya niangalie nani wa kuweza kutusaidia,naushukuru sana ubalozi wa China kwa kukubali kusaidia akina mama wa mkoa wa Shinyanga ili kupunguza vifo vya mama na watoto”,alieleza Hamad.
Alisema inasikitisha kuona akina mama na watoto wakipoteza maisha hivyo kuwataka wananchi kupiga vita mimba na ndoa za utotoni ili kuwaepusha kupoteza maisha wakati wa kujifungua.
Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) mkoa wa Shinyanga Masanja Salum alimshukuru mbunge huyo kwa kuwakumbuka akina mama huku akiomba viongozi wengine kujitokeza na kusaidia wananchi ili kuleta maendeleo katika jamii.
Naye mganga mkuu wa wilaya ya Shinyanga ,Dkt. Damas Nyansira alisema msaada huo wa vifaa utasaidia kupunguza kero kwa wagonjwa ambao walikuwa wanalazimika kulala chini kutokana na upungufu wa vitanda.
Na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hilal Hamad (CCM) akitoa msaada wa vifaa tiba katika kituo cha afya Tinde halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hilal Hamad (CCM) akiwa katika kituo cha afya Nhobola halmashauri ya wilaya ya Kishapu
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hilal Hamad (CCM) akiwa katika kituo cha afya Songwa kilichopo halmashauri ya wilaya ya Kishapu
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hilal Hamad (CCM) akiwa katika zahanati ya Solwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini.
Social Plugin