Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI WAHAMASISHA WAAJIRI KUJISAJILI-TAZAMA PICHA MAANDAMANO MEI MOSI 2017 MOSHI NA DAR ES SALAAM


Wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (Workers Compensation Fund – WCF), wameadhimisha siku ya wafanyakazi duniani 'Mei Mosi' kwa kushiriki maandamano na kutoa elimu katika Viwanja vya Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro huku wengine wakifanya matembezi kutoka Mnazi Mmoja hadi uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.


Kitaifa sherehe hizo zimeongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli mjini Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo alipokea maandamano ya wafanyakazi kutoka taasisi za umma na binafsi kisha kuwahutubia wafanyakazi.

Akizungumza kwenye sherehe za Mei Mosi mkoani Kilimanjaro Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi - WCF, Masha Mshomba, amewahamasisha waajiri nchini kujisajili katika mfuko huo kwani mfuko huo ni mkombozi mkubwa kwa waajiri na wafanyakazi. 


"Mfuko wa Fidia ni mkombozi kwa waajiri na wafanyakazi nchini kwa sababu umekuja katika kipindi ambacho huko nyuma tulikuwa hatuna chombo hiki,wafanyakazi walikuwa wakipata ajali na magonjwa yanayotokana na 
kazi bila kupata fidia sasa mfuko umekuja mambo hayo yatakuwa historia",alieleza Mshomba.


Mshomba alisema WCF ni faraja kwa waajiri kwani utawawezesha kujikita katika uzalishaji tu, na WCF kubaki na jukumu la kumuhudumia mfanyakazi anapoumia au kuugua.

Alisema pamoja na kwamba waajiri ndiyo wachangiaji wakuu,mfuko wa WCF umewaondolea mzigo wa kuhangaika na mtumishi pale anapopata ajali, au maradhi yatokanayo na kazi anazofanya. 

“Tunawasihi sana waajiri waendelee kujisajili katika mfuko wa WCF kwa haraka kabisa ili waweze kunufaika wao na wafanyakazi wao,mfanyakazi akipata ajali atapata huduma ya matibabu na kama amepata ulemavu basi atapata fidia katika malipo ya pensheni ya kila mwezi”,aliongeza Mshomba. 

Mgeni rasmi katika sherehe za Mei Mosi jijini Dar es Salaam, alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeka, Bw.Felix Lyaviva, ambaye alipokea maandamano ya wafanyakazi na magari kadhaa kutoka taasisi za umma na binafsi yakionesha huduma zitolewazo na taasisi hizo.

Kauli mbiu ya Siku ya Wafanyakazi duniani mwaka huu ni “Uchumi wa Viwanda uzingatie Haki, Maslahi na Heshima ya wafanyakazi”.

WCF ni Mfuko ulioanzishwa kwa sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi namba 20 ya mwaka 2008 na ndiYo Mfuko unaowajibika kutoa Mafao ya Fidia kwa Wafanyakazi walioumia au kupatwa na maradhi yaliyosababishwa na kazi wanazozifanya lakini pia kutoa Fidia kwa wategemezi pindi Mfanyakazi anapofariki kwa kuzingatia vigezo
vilivyowekwa.

Tumekusogezea picha wakati wa sherehe za Mei Mosi mwaka 2017 mkoani Kilimanjaro na Dar es salaam.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog Moshi na Khalfan Said wa K-VIS BLOG - Dar es salaam
Kilimanjaro- Wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (Workers Compensation Fund – WCF) wakiwa katika maandamano
Rais John Pombe Magufuli akipokea maandamano ya wafanyakazi wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani 'Mei Mosi' mwaka 2017 katika viwanja vya Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro
Wafanyakazi kutoka Mfuko wa WCF wakiwa katika banda la WCF wakati wa maadhimisho ya sherehe za Mei Mosi mwaka 2017 ambapo wananchi walipata fursa ya kupata elimu kuhusu mfuko huo
Wananchi wakiwa katika banda la WCF
Wananchi wakiwa katika banda la WCF wakipata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa mfuko huo
Wafanyakazi wa mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi -WCF wakibadilishana mawazo baada ya sherehe za Mei Mosi kumalizika katika viwanja vya Ushirika Moshi mkoani Moshi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu na Tathmini WCF, Dkt. Abdulssalaam Omary,katikati ni Rajabu Ruje,kulia ni Afisa Uhusiano WCF, Zaria Mmanga.
Dar es salaam-Baadhi ya wafanyaakzi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), wakiungana na wenzao katika maandamano ya kuadhimisha siku ya Wafanyakazi Duniani ambapo kiraifa yamefanyika kwenya uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.







Maandamano yanaendelea
Waandamanaji wakiwa wamebeba bango

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog Moshi na Khalfan Said wa K-VIS BLOG - Dar es salaam

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com