Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWANASIASA ANYONYESHA MTOTO BUNGENI...SHUHUDIA HAPA

Seneta wa Australia Larissa Waters amekuwa mwanasiasa wa kwanza kunyonyesha katika bunge la taifa hilo.

Seneta wa Australia Larissa Waters amekuwa mwanasiasa wa kwanza kunyonyesha katika bunge la taifa hilo.

Bi Waters kutoka chama cha mrengo wa kushoto cha Green Party alimnyonyesha mwanawe wa miezi miwili Alia Joy wakati wa kura siku ya Jumanne.

Bunge mwaka uliopita lilijiunga na seneti kuruhusu kunyonyesha, lakini hakuna mbunge ambaye alikuwa amewahi kufanya hivyo.

Hatua hiyo inajiri baada ya Kelly O'Dwyer, waziri wa serikali 2015 kutakiwa kutoa maziwa ili kutokosa vikao vya bunge.

''Tunataka wanawake zaidi na wazazi bungeni'', bi Waters alisema katika mtandao wake wa facebook.

''Na tunahitaji mazingira bora katika maeneo ya kazi kwa uangalizi mzuri wa watoto kwa kila mtu''.

Seneta wa Leba Katy Gallagher alisema kuwa wakati huo unapaswa kutambuliwa.

''Wanawake wamekuwa wakinyonyesha katika mabunge tofauti duniani'', aliamba chombo cha habari cha Skynews Australia.

'''Wanawake wataendelea kuwa na watoto na iwapo wanataka kufanya kazi zao na wawe kazini na kuangalia watoto wao...basi bila shaka ukweli ni kwamba tutalazimika kuwapatia haki yao''.

Hadi kufikia mwaka uliopita, wabunge katika bunge dogo walikuwa wanaweza kuwabeba watoto wao na kuingia katika afisi za bunge pekee ama maeneo ya uma.

Wanasiasa wameruhusiwa kunyonyesha katika bunge la seneti tangu 2003.

Wazo hilo ni swala tata katika mabunge mengi duniani.

Mnamo mwaka 2016, mbunge wa Uhispania Carolina Bescansa kutoka chama cha Podemos alikosolewa na kupongezwa wakati huohuo kwa kumpeleka mwanawe bungeni na kumnyonyesha.
Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com