Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NAHODHA WA TIMU YA SIMBA JONAS MKUDE APATA AJALI MOROGORO

Siku moja baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali ya Kombe la Azam Sports Federation Cup kati ya Simba dhidi ya Mbao FC katika uwanja wa Jamhuri Dodoma na Simba kuibuka na ushindi wa magoli 2-1, leo May 28 nahodha wa timu hiyo Jonas Mkude ameripotiwa kupata ajali.

Jonas Mkude
Mkude ambaye alikuwa katika gari binafsi na baadhi ya watu amepata ajali ya gari akitokea Dodoma akiwa maeneo ya Dumila mkoani Morogoro akiwahi Dar es Salaam kwa ajili ya kambi ya timu ya taifa Taifa Stars.

Gari waliyopata nayo ajali Jonas Mkude na abiria wengine

Taarifa za awali zinaeleza kuwa Mkude ameumia maeneo ya shingo na amepelekwa hospitali wakati mmoja kati ya abiria waliyokuwemo katika gari hilo akiripotiwa kupoteza maisha 

Kutoka Kushoto ni beki wa Simba Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ shabiki na Said Ndemla kiungo wa Simba SC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com