Moja ya stori ambazo sikuwahi kufahamu ni juu ya hizi sheria za jamii mbalimbali duniani ambazo zinaweza kushtua kushangaza wengi wanaozisikia, kuzisoma ambapo kwa wale waliobahatika kuzitembelea sehemu hizi, basi ni mashuhuda.
1. Sudan
Katika nchi ya Sudan, hasa katika kabila la Latuka, kama mwanaume anataka kumuoa mwanamke, anamteka. Mwanaume huyo anaweza kuomba ruhusa ya baba kwanza ambaye kama atakataa, atalazimisha kumuoa mwanamke.
2.Ujerumani
Kabla ya ndoa nchini Ujerumani, hufanywa kwanza sherehe ya polterabend. Ni sherehe ambayo hufanywa na wanandugu kwa kutupa uchafu sehemu ambayo patafanyika harusi ili wanandoa wapafanyie usafi. Kitendo hiki kinatafsiriwa kuwa ugumu wa maisha watakayoishi kwenye ndoa. Panaweza kutupwa chochote isipokuwa vioo.
3,Iran
Nchini Iran, kama mtu atakupa kitu chochote (chakula, zawadi n.k), unatakiwa ukatae mara tatu kabla ya kukubali kupokea. Kufanya kinyume chake huhesabiwa ni kitendo kibaya.
4.Brazil
Katika kabila la Satere-Mawe, Brazil, mtoto wa kiume anapotimiza umri wa miaka 12, atakuwa mwanaume kamili kwa kuweka mikono yake sehemu maalumu iliyowekwa siafu ambao watamng’ata kwa dakika 10.
5.Venezuela
Makabila ya Yanomami (asili yake Venezuela), mmoja anapofariki, ndugu zake hula majivu yao wakiamini wanaifanya nafsi ya marehemu ihifadhiwe pema na mapepo mabaya hukaa mbali na maiti.
6.Ugiriki
Ugiriki, ni lazima kwa wagiriki kusema “piase kokkino” watu wawili wanapotamka neno moja kwa wakati mmoja. Kitu kama hicho hutokea kama mtu atamuona paka mweusi: atalazimika kutema mate mara tatu. Kama hatofanya hivyo, kitu kibaya kitamtokea.
7.Austria
Nchini Austria, wana Santa Klaus wao anaitwa Krampus ambaye hupita mitaani kuwatisha watoto ambao hutajwa kuwa na tabia mbaya. Utamduni huu hufanywa wiki ya kwanza ya December.