Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YAGHARAMIA MSIBA WA WANAFUNZI WALIOFARIKI ARUSHA.... KUFANYIWA IBADA UWANJA WA SHEIKH AMRI ABEID

Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania imegharamia Sanda pamoja na majeneza kwa ajili ya Wanafunzi wa Shule ya Lucky Vicent waliopoteza maisha mapema jana kwenye ajali iliyokuwa ikihusisha safari ya kimasomo.


Akitoa taarifa hiyo leo Meya wa Jiji la Arusha , Mh. Calist Lazaro amesema kuwa taarifa za awali zinaonyesha kuwa tayari Serikali imekwishalipia gharama za majeneza na sanda ya kuhifadhia miili ya marehemu ambao kesho wanatarajiwa kufanyiwa ibada katika Uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com