Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA) limempongeza mheshimiwa rais John Pombe Magufuli kwa hatua alizozochukua baada ya kupokea ripoti ya uchunguzi wa mchanga wenye madini ambapo miongoni mwa maamuzi yaliyochukuliwa na rais ni kusitisha usafirishaji wa mchanga huo nje ya nchi.
Pongezi hizo zimetolewa leo na rais wa shirikisho hilo John Bena wakati akiongea na waandishi wa habari na viongozi mbalimbali wa wachimbaji wadogo wa madini.
Bena amesema uamuzi uliochukuliwa na rais Magufuli utasaidia nchi kupata faida kwa madini ambayo yalikuwa yakichukuliwa bila kufahamu kuwa kuna madini mengine ndani yake.
Kwa upande wake mtendaji mkuu wa FEMATA Haroun Kinega akiwataka wachimbaji wadogo kuunga mkono juhudi za mheshimiwa rais Magufuli.
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Wachimbaji Madini mkoa wa Singida Robert Marando amesema hatua alizo chukua rais Magufuli zitawasaidia wachimbaji wadogo kupata faida,kwani walikuwa wakishafirisha shaba nje ya nchi huku ikiwa na madini mengine.
Imeandaliwa na Raymond Herman wa Malunde1 blog
Social Plugin