Shule ya Lucky Vicent imefungwa kwa siku saba kufuatia vifo vya wanafunzi wake zaidi ya 30 vilivyotokea kwenye ajali ya gari jana Karatu mkoani Arusha.
Kutokana na ajali hiyo Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na wabunge wengine wa Chadema wamefika shuleni hapo kutoa pole.
Lema kwa niaba wabunge ameeleza kusikitishwa na msiba huu na amewapa pole wafiwa lakini akatoa angalizo kusiingizwe siasa katika msiba huu mkubwa.
Meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro ameeleza kuwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene na Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako watafika jioni kuzungumza na wafiwa.
Kesho Makamu wa Rais Samia Suluhu kwa niaba ya Rais John Magufuli ataongoza kazi kuaga miili ya wanafunzi hao Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Mkuu wa shule hiyo, Ephraem Jackson amesema hadi sasa vifo ni 36 na wanafunzi wawili bado wamelazwa Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru. Wanafunzi hao ni Sadiely Ismail na Wilson Tarimo.
Social Plugin