Leo May 25, 2017 zimeripotiwa taarifa za kifo cha Ivan Semwanga “Ivan Don” mfanyabiashara maarufu kutoka nchini uganda na aliyekuwa mume wa mrembo Zari the Boss Lady, ambaye amefariki baada ya kuugua ghafla takriban wiki moja sasa.
Taarifa za kifo cha Ivan zimethibitishwa na Zari ambaye alizaa naye watoto watatu wa kiume, alikuwa akijulikana zaidi kutokana na kuwa na uwezo mkubwa kifedha, aina ya maisha aliyokuwa akiishi ikiwemo kutoa misaada ya fedha kila mwezi kwa watu wenye matatizo mbalimbali.
Nimekuwekea post ya mwisho ya Ivan aliyoiweka Instagram muda mfupi kabla ya kuanza kuumwa hadi kifo kinamkuta.
Social Plugin