Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack amekanusha taarifa zinazosambaa kwa kasi mtandaoni kuwa amezuiwa kuingia katika mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu uliopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Akizungumza na Malunde1 blog,mheshimiwa Telack ameeleza namna ilivyokuwa:
“Ilikuwa ni ziara ya Kushtukiza kwa sababu kule mgodini wanatoka watu wa TMAA ambao wanakaa kule mgodini kwa niaba ya serikali ambao wanatakiwa wahojiwe,kwa hiyo watu wote wakatakiwa waondolewe mgodini,migodi sasa ikabaki haina uwakilishi wa serikali”,
“Kama mkoa tukasema kama hakuna mwakilishi wa serikali maana yake ni zamu yetu kuweka lindo la kwetu,lazima tukahakikishe kwamba migodi hiyo iko salama kwa maana ya kile kinachozalishwa kwani migodi inaweza kutumia mwanya huo kusafirisha dhahabu ambayo wameshaitengeneza”.
“Pamoja na kwamba tuliweka walinzi jana,tumeona ni vyema tukaangalie ambacho kipo hasa kilichozalishwa ni nini,kwa hiyo tukaanza na mgodi wa Buzwagi,tukaona dhahabu iliyozalishwa,wakatupeleka kwenye Chumba maalum cha dhahabu yaani "gold room",tukakuta mabaa ya dhahabu tukahesabu,tukayapima kujua yapo kiasi gani,tukawaambia kwa kuwa watu wa TMAA hawapo,wasitengenezee baa zingine mpaka pale serikali itakapoleta hao watu kwani hao ndiyo wanahakiki kile kinachozalishwa”,-Telack.
“Baada ya kutoka Buzwagi tukaenda Bulyanhulu,tumeingia vizuri mgodini mpaka kwenye gold room,tulipofika sasa tukashindwa kuingia mahali ambapo dhahabu inahifadhiwa,sababu waliyotoa ni kwamba walifungua asubuhi na wao wakishafunga huwa wanaset na muda kuwa kesho watafungua saa ngapi,kwa hiyo haiwezi kufunguka mpaka kesho".
"Tulichokifanya tumeacha ulinzi wa kutosha pale ili kuhakikisha kuwa dhahabu ambayo tayari imezalishwaa isiweze kusafirishwa kinyemela kwani watu wa TMAA hawapo,kwa hiyo tutarudi kesho ili kujua kiasi gani cha dhahabu kipo”-RC Telack.
"Tulichokifanya tumeacha ulinzi wa kutosha pale ili kuhakikisha kuwa dhahabu ambayo tayari imezalishwaa isiweze kusafirishwa kinyemela kwani watu wa TMAA hawapo,kwa hiyo tutarudi kesho ili kujua kiasi gani cha dhahabu kipo”-RC Telack.
Naye Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Acacia ambayo ndiyo
wamiliki wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu, Nekta Foya,amesema mkuu wa mkoa
alifika na kupokewa vyema katika mgodi wa Bulyanhulu na kupewa ushirikiano wote
hadi kuingia ndani ya chumba cha dhahabu (gold room), lakini hakuingia katika
sefu ya dhahabu kutokana na muda aliofika kuwa imejifunga.
“Unajua kwa ajili ya usalama, unaweza kuingia chumba cha
dhahabu, usifike kwenye dhahabu kwa kuwa hufungwa kwa muda maalumu kutokana na
mipango ya uzalishaji, sasa muda ambao amefika mfumo wetu wa usalama (time
lock) wa sefu ya dhahabu, ulikuwa umejifunga, usingeweza kufunguka hadi kesho ”
- Foya.
Amesema baada ya kufahamishwa na maofisa wao waliokuwapo, RC
Zainabu alikubalina nao na kupanga kuendelea kesho na ukaguzi wake, lakini
kutokana na kutaka uhakika zaidi mkuu wa mkoa aliacha askari kulinda eneo hilo.
TAARIFA KUTOKA OFISI YA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA
Habari za jioni, taarifa zinazosambaa kuwa Mhe Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack amezuiwa kuingia mgodini Bulyanhulu.
Taarifa hizo si za kweli. Mhe. Mkuu wa Mkoa ametembelea migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu leo kujionea shughuli za uzalishaji bila kuwepo maafisa wa TMAA.
Baada ya kuona uzalishaji ameagiza uyeyushaji wa dhahabu "melting" usiendelee bila kuwepo maafisa hao.
Taarifa hizo si za kweli. Mhe. Mkuu wa Mkoa ametembelea migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu leo kujionea shughuli za uzalishaji bila kuwepo maafisa wa TMAA.
Baada ya kuona uzalishaji ameagiza uyeyushaji wa dhahabu "melting" usiendelee bila kuwepo maafisa hao.
Katika mgodi wa Bulyanhulu,mhe. Mkuu wa Mkoa ameagiza jeshi la Polisi kulinda Chumba maalum cha dhahabu yaani "gold room" kutokana na kushindikana kufunguliwa kwa madai kuwa kimefungwa kwa program maalum ya masaa 24.
Hivyo jeshi la Polisi linalinda eneo hilo hadi hapo kesho saa 12.00 asubuhi chumba hicho kitapofunguliwa na Mhe. Mkuu wa Mkoa atashuhudia.
Afisa Habari,
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Shinyanga.
25/05/2017.
Social Plugin