Wakazi wa Barabara ya Iloganzala Jijini Mwanza jana walipigwa butwaa baada ya mti aina ya mwembe kutoa sauti kama binadamu ukipinga using'olewe.
Tukio hilo limetafsiriwa kuwa la kishirikina ama mazingaombwe ikizingatiwa kwamba si jambo lenye uhalisia mti kuongea kama binadamu.
Katika eneo la Iloganzala Jijini Mwanza kuna upanuzi wa barabara inayoelekea Uwanja wa ndege wa Mwanza.
Shughuli ya kuung'oa mti huo aina ya mwembe leo imeendelea ikiwa ni siku ya pili ya kukabiliana na mwembe huo na hatimaye wamefanikiwa kuung'oa huku mamia ya wananchi wakishuhudia tukio hilo la ajabu.
Kwa mujibu wa maelezo kutoka wananchi wa eneo hilo wanasema jirani na mti huo kuna nyumba iliwahi iligoma kubomolewa wakati wa upanuzi wa barabara
Kwa mujibu wa maelezo kutoka wananchi wa eneo hilo wanasema jirani na mti huo kuna nyumba iliwahi iligoma kubomolewa wakati wa upanuzi wa barabara
Tazama Video hapa chini
Social Plugin