NB-picha kutoka maktaba siyo ya waandishi waliokamatwa
Habari zilizotufikia hivi punde kutoka mkoani Arusha ni kwamba waandishi wa habari 9 wamekamatwa na polisi wakati wakitekeleza majukumu yao.
Inaelezwa kuwa waandishi wamekamatwa na jeshi la polisi Arusha kwa madai ya kuhudhuria kikao ambacho hakikuwa na kibali katika shule ya Lucky Vincent ambapo shirikisho la wamiliki wa shule binafsi walikuwa wanaenda kutoa rambirambi lakini baada ya kupata taarifa walienda kufanya kazi ndipo wakaambulia kukamatwa na polisi

Inaelezwa kuwa mbali na waandishi wa habari kukamatwa pia Meya wa Jiji la Arusha Mstahiki Kalisti Lazaro, Wamiliki wa shule, Viongozi wa dini nao wamekamatwa katika eneo la shule ya Lucky Vicent Arusha walipokuwa wamekwenda kutoa rambirambi.
Waandishi wa habari waliokamatwa na polisi
Waandishi wa habari waliokamatwa na polisi
1 .Godfrey Thomas -Ayo Tv
2.Alphonce Saul Kusaga- Triple A
3.Filbert Rweyemamu- Mwananchi
4.Hussein Tuta Itv
5.Joseph Ngilisho-Sunrise radio
6.Geofrey Stephen- Radio 5
7.Janeth Mushi -Mtanzania
8.Zephania Ubwani- The Citizen
9.Elihuruma Yohani- Tanzania Daima
10.Idd Uwesu -Azam Tv